Shurba Ya Nyama Mbuzi Ya Ngano Za Kukobolewa Na Ya Kotimiri
Shurba Ya Nyama Mbuzi Ya Ngano Za Kukobolewa Na Ya Kotimiri
Vipimo
Nyama ya mbuzi – kilo 1
Ngano zilokobolewa (Quacker oats) – kikombe 1 cha chai
Kitunguu maji kilosagwa - 3
Nyanya ilosagwa – 1
Kitunguu thomu kilosagwa – vijiko 2 vya supu
Tangawizi ilosagwa – vijiko 2 vya supu
Mdalasini – kijiti 1
Pilipili manga - kijiko 1 cha chai
Jira/uzile (cummin powder) – vijiko 2 vya chai
Gilgilani/Dania (coriander)
Kotmiri – msongo 1
Ndimu – vijiko 2 vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Weka nyama katika sufuria ya kupikia. Tia thomu, tangawizi, chumvi, bizari zote.
- Tia maji kiasi uchemshe nyama hadi iwive kiasi dakika 45
- Tia kitunguu, nyanya endelea ichemke viwive
- Changanya ngano katika maji kidogo kwenye kibakuli, kisha mimina katika shurba uendelee kupika kidogo tu kiasi dakika 10
- Tia kotimiri uliokatakata, koroga uchanganye
- Tia ndimu ikiwa tayari kuliwa
- Unapopakuwa katika kibakuli, nyunyizia kotimiri
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)