064-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango wa Ubora wa Tajiri Mwenye Kushukuru na Kuchuma Mali na Halali na Kuitumia kwa Njia Iliyoamriwa
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل الغَنِيّ الشاكر وهو من أخذ المال من وجهه وصرفه في وجوهه المأمور بِهَا
064-Mlango wa Ubora wa Tajiri Mwenye Kushukuru na Kuchuma Mali na Halali na Kuitumia kwa Njia Iliyoamriwa
قَالَ الله تَعَالَى:
فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ ﴿٥﴾ وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٦﴾ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٧﴾
Basi yule anayetoa (mali) na akamcha Allaah. Na akasadikisha Al-Husnaa (jazaa na laa ilaaha illa Allaah). Basi Tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi [Al-Layl: 5-7]
وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى ﴿١٧﴾ الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّىٰ ﴿١٨﴾ وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰ ﴿١٩﴾ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَىٰ ﴿٢٠﴾ وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ ﴿٢١﴾
Na ataepushwa nao mwenye taqwa kabisa. Ambaye anatoa mali yake kujitakasa. Na hali hakuna mmoja yeyote aliyemfanyia fadhila yoyote hata amlipe. Isipokuwa kutaka Wajihi wa Rabb wake Aliyetukuka. Na bila shaka atakuja kuridhika. [Al-Layl: 17-21]
إِن تُبْدُوا الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِيَ ۖ وَإِن تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاءَ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّئَاتِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٧١﴾
Mkidhihirisha swadaqah basi ni vizuri hivyo, na mkizificha na kuwapa mafakiri, basi hilo ni khayr kwenu. Na Atakufutieni katika maovu yenu. Na Allaah kwa yale myatendayo, ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Al-Baqarah: 271]
لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٩٢﴾
Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachotoa basi hakika Allaah kwacho ni Mjuzi. [Aal-'Imraan: 92]
Hadiyth – 1
وعن عبدِ الله بن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ حَسَدَ إِلاَّ في اثْنَتَيْنِ : رَجُلٌ آتَاهُ اللهُ مَالاً ، فَسَلَّطَهُ عَلَى هَلَكَتِهِ فِي الحَقِّ ، وَرَجُلٌ آتَاهُ اللهُ حِكْمَةً فَهُوَ يَقضِي بِهَا وَيُعَلِّمُهَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hapana kuoneana wivu ila kwa mambo mawili: Mtu aliyepewa na Allaah mali na akawa akaitumia katika njia ya haki (kujikurubisha na Allaah pamoja na kutii) na mtu ambaye amepatiwa na Allaah hekima, naye anahukumu watu kwayo na kuifundisha." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لاَ حَسَدَ إِلاَّ في اثْنَتَيْنِ : رَجُلٌ آتَاهُ اللهُ القُرْآنَ ، فَهُوَ يَقُومُ بِهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَآنَاءَ النَّهَارِ ، وَرَجُلٌ آتَاهُ مَالاً ، فَهُوَ يُنْفِقُهُ آنَاءَ اللَّيْلِ وَآنَاءَ النَّهَارِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Na imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hapana hasad (wivu) ila kwa watu wawili: Mtu ambaye amepatiwa Quraan na Allaah, naye akawa amesimama imara nayo kwa kuisoma na kuitekeleza maamrisho yake mchana na usiku; na mwengine ni yule aliyepatiwa mali na Allaah, naye akawa anaitoa (swadaqah) mchana na usiku." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ فُقَراءَ المُهَاجِرينَ أتَوْا رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالُوا : ذَهَبَ أهْلُ الدُّثُورِ بِالدَّرَجَاتِ العُلَى ، وَالنَّعِيم المُقيم ، فَقَالَ : (( وَمَا ذَاك ؟)) فَقَالوا : يُصَلُّونَ كَمَا نُصَلِّي ، وَيَصُومُونَ كَمَا نَصُومُ ، وَيَتَصَدَّقُونَ وَلاَ نَتَصَدَّقُ ، وَيَعْتِقُونَ وَلاَ نَعْتِقُ ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( أفَلا أُعَلِّمُكُمْ شَيْئاً تُدْرِكُونَ بِهِ مَنْ سَبَقَكُمْ ، وَتَسْبِقُونَ بِهِ مَنْ بَعْدَكُمْ ، وَلاَ يَكُونُ أحَدٌ أفْضَلَ مِنْكُمْ إِلاَّ مَنْ صَنَعَ مِثْلَ مَا صَنَعْتُمْ ؟ )) قالوا : بَلَى يَا رسول الله ، قَالَ : (( تُسَبِّحُونَ وَتُكَبِّرُونَ وَتَحْمِدُونَ ، دُبُرَ كُلِّ صَلاَةٍ ثَلاثاً وَثَلاثِينَ مَرَّةً )) فَرَجَعَ فُقَرَاء المُهَاجِرِينَ إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فقالوا : سَمِعَ إخْوَانُنَا أهلُ الأمْوالِ بِمَا فَعَلْنَا ، فَفَعَلُوا مِثلَهُ ؟ فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( ذَلِكَ فَضْلُ اللهِ يُؤْتِيهِ مَنْ يَشَاءُ )) متفقٌ عَلَيْهِ ، وَهَذا لفظ رواية مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba mafakiri wa Muhaajirina walikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: "Wenye mali nyingi wamenyakuwa daraja za juu na neema za daima." Akasema: "Na inakuwa vipi hilo?" Wakasema: "Wao wanaswali kama tunavyoswali, wanafunga kam tunavyofunga, wanatoa swadaqah nasi hatutoi, wanaacha watumwa wala hatuachi." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Je niwafundishe kitu mtawafikia nacho waliowapiteni, na mtawashinda wa baada yenu, wala hakuna bora kuliko nyinyi ila atakayefanya mnavyofanya?" Wakasema: "Ndio ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Msabihini Allaah, Muhimidini Allaah na leteni takbiri baada ya kila Swalaah mara thelathini na tatu." Walirudi tena mafakiri wa Muhaajirina kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakasema: 'Ndugu zetu wenye mali wamesikia tunayofanya, wakafanya mfano wake?" Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hiyo ni fadhila ya Allaah anampa amtakaye." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya riwaayah ya Muslim]