066-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kuzuru Makaburi kwa Wanaume na Anachosema Mwenye Kuzuru
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب زيارة القبور للرجال وما يقوله الزائر
066-Mlango Wa Kupendeza Kuzuru Makaburi kwa Wanaume na Anachosema Mwenye Kuzuru
Hadiyth – 1
عن بُرَيْدَة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( كُنْتُ نَهَيْتُكُمْ عن زِيَارَةِ القُبُورِ فَزُوروها )) رواه مسلم .
وفي رواية : (( فَمَنْ أرَادَ أنْ يَزُورَ القُبُورَ فَلْيَزُرْ ؛ فإنَّهَا تُذَكِّرُنَا الآخِرَةَ )) .
Imepokewa kutoka kwa Buraydah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nilikuwa nimekukatazeni kuzuru makaburi, sasa yazuruni." [Muslim]
Na katika riwaayah: "Yeyote anayetaka kuzuru makaburi basi ayazuru; kwani (huko kuzuru makaburi) kutawakumbusha Aakherah."
Hadiyth – 2
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم - كلَّما كَانَ لَيْلَتُهَا مِنْ رسول الله صلى الله عليه وسلم - يَخْرُجُ مِنْ آخِرِ اللَّيْلِ إِلَى البَقِيعِ ، فَيقولُ : (( السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ دَارَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ ، وَأتَاكُمْ مَا تُوعَدُونَ ، غَداً مُؤَجَّلْونَ ، وَإنَّا إنْ شَاءَ اللهُ بِكُمْ لاَحِقُونَ ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لأهْلِ بَقِيعِ الغَرْقَدِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kila inapokuwa zamu yake, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), alikuwa anatoka mwisho wa usiku kuelekea Baqii' na anasema: "Amani juu yenu Waumini wa nyumba hii, Yamekujieni mlioahidiwa, Mmetangulizwa wakatimaalumu. Na hakika sisi akitaka Allaah tutakutana nanyi. Ee Mola wangu wasamehe watu wa Al'Baqi'i Al-Gharqad, (yenye michongoma)." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن بريدة رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم يُعَلِّمُهُمْ إِذَا خَرَجُوا إِلَى المَقَابِرِ أنْ يَقُولَ قَائِلُهُمْ : (( السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ أهلَ الدِّيَارِ مِنَ المُؤْمِنينَ وَالمُسلمينَ ، وَإنَّا إنْ شَاءَ اللهُ بِكُمْ للاَحِقونَ ، أسْألُ اللهَ لَنَا وَلَكُمُ العَافِيَةَ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Buraydah (Radhwiya Allahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwafundisha dua wakitoka kwenda makaburini asema mmoja wao: "Amani juu yenu watu wa nyumba hizi miongoni mwa Waumini na Waislamu. Na hakika sisi akitaka Allaah tutakutana nanyi, Tunamuomba Allaah sisi na nyinyi afya." [Muslim]
Hadiyth – 4
وعن ابن عباسٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : مرَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم بِقُبورٍ بالمدِينَةِ فَأقْبَلَ عَلَيْهِمْ بِوَجْهِهِ ، فَقَالَ : (( السَّلامُ عَلَيْكُمْ يَا أهْلَ القُبُورِ ، يَغْفِرُ اللهُ لَنَا وَلَكُمْ ، أنْتُمْ سَلَفُنَا وَنَحنُ بالأثَرِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Na imepokewa kutoka kwa bn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita katika makaburi ya Madiynah akayakabili kwa uso wake na kusema: "Amani iwashukie enyi watu wa makaburi. Allaah atusamehe sisi na nyinyi. Nyinyi mumetutangulia nasi tunawafuatia." [At-Tirmidhiy, na kasema ni Hadiyth Hasan].