08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Swiyaam: Nguzo Ya Swiyaam
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swiyaam
08-Nguzo Ya Swiyaam
Ni kujizuia na yenye kufunguza toka kuchomoza Alfajiri hadi Magharibi. Allaah Ta’aalaa Amesema:
((فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ))
((Basi sasa waingilieni na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku). Kisha timizeni Swiyaam mpaka usiku)). [Al-Baqarah (2:187)]
Allaah Ta’aalaa Ameruhusu idadi hii ya mambo yenye kufunguza usiku wa Swiyaam, kisha Akaamuru kujizuia nayo mchana wake. Hivyo basi, Ametutaarifu kuwa uhalisia wa Swawm na mhimili wake ni kujizuia. [Tuhfat Al-Fuqahaa (1/537)na Badaai’u As-Swanaai’ i (2/90)]