01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Hajj Na 'Umrah: Taarifu Ya Hajj
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Hajj Na ‘Umrah
01-Taarifu Ya Hajj
Asili ya maana ya Al-Hajji (الحجُّ) katika lugha, ni kukusudia. Ni kwa kufatahisha “Haa”, na inajuzu kwa kasrah “Al-Hijju”, nayo ni nadra sana. Inasemekana kuwa inatokana na neno lako: (حججتُه) unapomwendea mtu mara kwa mara. Na inasemekana kuwa kinyume na hilo, na la kwanza ndilo mashuhuri. [Taaj Al-‘Aruws na Al-Majmuw’u (7/7)]
Ama katika istilahi ya kisharia, ni kuikusudia Nyumba Tukufu ya Allaah na Maeneo Maalum ya Kutekelezea amali na ‘ibaadah maalum za Hajji katika wakati maalum, na kwa namna maalum.