03-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: Baadhi Ya Sifa Za Allaah (عز وجل) Zilizotajwa Katika Qur-aan

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

03-Baadhi Ya Sifa Za Allaah (عز وجل) Zilizotajwa Katika Qur-aan

 

 

 

 

أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ

Mwadilifu Zaidi Wa Wanaohukumu Kuliko Mahakimu Wote.

 

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَنَادَىٰ نُوحٌ رَّبَّهُ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ابْنِي مِنْ أَهْلِي وَإِنَّ وَعْدَكَ الْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ﴿٤٥﴾

Na Nuwh akamwita Rabb wake, akasema: Rabb wangu! Hakika mwanangu ni katika ahli zangu, na hakika ahadi Yako ni ya kweli, Nawe ni Mwadilifu zaidi wa wanaohukumu kuliko mahakimu wote.  [Huwd (11): 45]

 

 

 

أَهْلُ الْمَغْفِرَةِ

Mstahiki Wa Kughufuria (Madhambi)

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ هُوَ أَهْلُ التَّقْوَىٰ وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ﴿٥٦﴾

Na hawatowaidhika isipokuwa Akitaka Allaah; Yeye Ndiye Mstahiki wa kuogopwa, na Mstahiki wa kughufuria (madhambi).  [Al-Muddath-thir (74): 56]

 

 

 

 

عالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ

Mjuzi Wa Ghayb Na Dhahiri

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ وَيَوْمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُ ۚ قَوْلُهُ الْحَقُّ ۚ وَلَهُ الْمُلْكُ يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ ۚ عالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿٧٣﴾

Naye Ndiye Ambaye Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Na Siku Atakaposema: Kun! basi (jambo) huwa! Kauli Yake ni haki.  Naye Atakuwa na ufalme Siku itakapopulizwa baragumu. Mjuzi wa ghayb na dhahiri. Naye ni Mwenye hikmah wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.  [Al-An-‘Aam (6): 73]

 

 

 

عَلَّامُ الْغُيُوبِ

Mjuzi Wa Ghayb

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَوْمَ يَجْمَعُ اللَّـهُ الرُّسُلَ فَيَقُولُ مَاذَا أُجِبْتُمْ ۖ قَالُوا لَا عِلْمَ لَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١٠٩﴾

Siku Allaah Atakayowakusanya Rusuli na Kuwaambia: Mlijibiwa nini? Watasema: Hatuna ujuzi nalo; hakika Wewe Ndiye Mjuzi wa ghayb. [Al-Maa-idah (5): 109]

 

 

 

أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ

Mbora Zaidi Wa Kurehemu

Kuliko Wengine Wote Wenye Kurehemu

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِأَخِي وَأَدْخِلْنَا فِي رَحْمَتِكَ ۖ وَأَنتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿١٥١﴾

 (Muwsaa) Akasema: Rabb wangu! Nighufurie na kaka yangu, na Utuingize katika rahmah Yako. Nawe ni Mbora zaidi wa kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu. [Al-A’raaf (7) 151]

 

 

 

 

أَسْرَعُ الْحَاسِبِينَ

Mwepesi Zaidi Kuliko Wote Wanaohisabu

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

ثُمَّ رُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۚ أَلَا لَهُ الْحُكْمُ وَهُوَ أَسْرَعُ الْحَاسِبِينَ ﴿٦٢﴾

Kisha hurudishwa kwa Allaah Rabb wao wa haki. Tanabahi! Hukumu ni Yake Pekee; Naye ni Mwepesi zaidi kuliko wote wanaohisabu. [Al-An’Aam (6): 62]

 

 

 

 

ذُو الْعَرْشِ

Mwenye ‘Arsh

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

رَفِيعُ الدَّرَجَاتِ ذُو الْعَرْشِ يُلْقِي الرُّوحَ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ لِيُنذِرَ يَوْمَ التَّلَاقِ﴿١٥﴾

 (Allaah) Mwenye uluwa juu ya vyeo na daraja. Mwenye ‘Arsh, Anapelekea Ar-Ruwh (Wahy) kwa amri Yake kwa Amtakaye miongoni mwa waja Wake, ili aonye Siku ya kukutana. [Ghaafir (40): 15]

 

 

 

 

ذُو فَضْلٍ

Mwenye Fadhila

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ خَرَجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَهُمْ أُلُوفٌ حَذَرَ الْمَوْتِ فَقَالَ لَهُمُ اللَّـهُ مُوتُوا ثُمَّ أَحْيَاهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ ﴿٢٤٣﴾

Je, hukuwaona wale walitoka majumbani mwao nao wakiwa ni maelfu wakikhofu mauti, Allaah Akawaambia: Kufeni kisha Akawahuisha? Hakika Allaah ni Mwenye fadhila juu ya watu lakini watu wengi hawashukuru.  [[Al-Baqarah (2): 243]

 

 

 

ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ

Mwenye Fadhila Adhimu

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٧٤﴾

Humchagua kwa rahmah Yake Amtakaye; na Allaah ni Mwenye fadhila adhimu. [Aali ‘Imraan (3): 74]

 

 

 

 

 

ذُو انتِقَامٍ

Mwenye Kulipiza

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْتُلُوا الصَّيْدَ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۚ وَمَن قَتَلَهُ مِنكُم مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاءٌ مِّثْلُ مَا قَتَلَ مِنَ النَّعَمِ يَحْكُمُ بِهِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ هَدْيًا بَالِغَ الْكَعْبَةِ أَوْ كَفَّارَةٌ طَعَامُ مَسَاكِينَ أَوْ عَدْلُ ذَٰلِكَ صِيَامًا لِّيَذُوقَ وَبَالَ أَمْرِهِ ۗ عَفَا اللَّـهُ عَمَّا سَلَفَ ۚ وَمَنْ عَادَ فَيَنتَقِمُ اللَّـهُ مِنْهُ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٩٥﴾

Enyi walioamini! Msiue mawindo na hali mko katika ihraam. Na atakayemuua (mnyama) miongoni mwenu kwa kusudi, basi malipo yake itakuwa ni kilicho sawa na alichokiua katika wanyama wa mifugo. Kama wanavyohukumu wawili wenye uadilifu miongoni mwenu. Mnyama huyo afikishwe Ka’bah, au kafara ya kulisha maskini, au badala ya hayo, kufunga swiyaam ili aonje matokeo maovu ya jambo lake. Allaah Ameshasamehe yaliyopita; na yeyote atakayerudia tena, basi Allaah Atamlipiza (kumuadhibu). Na Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kulipiza.  [Al-Maa-idah (5): 95]

 

 

 

ذُو عِقَابٍ أَلِيمٍ

Mwenye Adhabu Iumizayo.

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

مَّا يُقَالُ لَكَ إِلَّا مَا قَدْ قِيلَ لِلرُّسُلِ مِن قَبْلِكَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغْفِرَةٍ وَذُو عِقَابٍ أَلِيمٍ﴿٤٣﴾

Huambiwi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa yale yale waliyokwisha ambiwa Rusuli kabla yako. Hakika Rabb wako ni Mwenye maghfirah na Mwenye adhabu iumizayo. [Fusswilat (41: 43]

 

ذو المعارج

Mwenye Kumiliki Njia Za Kupandia

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ﴿١﴾ لِّلْكَافِرِينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ﴿٢﴾ مِّنَ اللَّـهِ ذِي الْمَعَارِجِ﴿٣﴾

 

Muulizaji ameuliza kuhusu adhabu itakayotokea. Kwa makafiri, ambayo hakuna wa kuikinga. Kutoka kwa Allaah Mwenye kumiliki njia za kupandia.   [Al-Ma’aarij (70: 1 - 3]

 

 

 

ذُو مَغْفِرَةٍ

Mwenye Maghfira

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِالسَّيِّئَةِ قَبْلَ الْحَسَنَةِ وَقَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِمُ الْمَثُلَاتُ ۗ وَإِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغْفِرَةٍ لِّلنَّاسِ عَلَىٰ ظُلْمِهِمْ ۖ وَإِنَّ رَبَّكَ لَشَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٦﴾

  Na wanakuhimiza kwa maovu kabla ya mazuri, na hali imekwishapita kabla yao mifano ya adhabu. Na hakika Rabb wako ni Mwenye maghfirah kwa watu juu ya dhulma zao, na hakika Rabb wako ni Mkali wa kuakibu. [Ar-Ra’d (13): 6]

 

 

 

 

ذُو الْقُوَّةِ

Mwenye Nguvu

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ ﴿٥٨﴾

Hakika Allaah Ndiye Mwingi wa kuruzuku, Mwenye nguvu Madhubuti.  [Adh-Dhaariyyaat (51): 58]

 

 

 

 

ذُو الرَّحْمَةِ ۚ

Mwenye Rahmah

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَرَبُّكَ الْغَنِيُّ ذُو الرَّحْمَةِ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَسْتَخْلِفْ مِن بَعْدِكُم مَّا يَشَاءُ كَمَا أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّيَّةِ قَوْمٍ آخَرِينَ ﴿١٣٣﴾

Na Rabb wako ni Mkwasi Mwenye rahmah. Akitaka Atakuondosheni na Aweke wengine watakaofuatia baada yenu kwa Atakao, kama vile Alivyokuzalisheni kutokana na vizazi vya watu wengine.  [Al-An’aam (6): 147]

 

 

 

ذُو الطَّوْلِ

Mwenye Wingi Wa Ukarimu

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

غَافِرِ الذَّنبِ وَقَابِلِ التَّوْبِ شَدِيدِ الْعِقَابِ ذِي الطَّوْلِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ إِلَيْهِ الْمَصِيرُ﴿٣﴾

Mwenye kughufuria dhambi, Anayepokea tawbah, Mkali wa kuakibu, Mwenye wingi wa Ukarimu, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake ndio mahali pa kuishia.  [Ghaafir (40): 3]

 

 

 

 

 

فَالِقُ الْحَبِّ وَالنَّوَىٰ

Mpasuaji Wa Mbegu Na Kokwa

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ اللَّـهَ فَالِقُ الْحَبِّ وَالنَّوَىٰ ۖ يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَمُخْرِجُ الْمَيِّتِ مِنَ الْحَيِّ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٩٥﴾

Hakika Allaah ni Mpasuaji wa mbegu na kokwa (zikawa miche). Anatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu na Mtoaji kilicho mfu kutokana na kilicho hai. Huyo Ndiye kwenu Allaah. Basi vipi mnaghilibiwa?   [Al-An’aam (6): 95]

 

 

 

 

 

فَاطِرُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

Muanzilishi Wa Mbingu Na Ardhi

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَتَّخِذُ وَلِيًّا فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ يُطْعِمُ وَلَا يُطْعَمُ ۗ قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَسْلَمَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٤﴾

Sema: Je, nimfanye mlinzi asiyekuwa Allaah; Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Naye Ndiye Anayelisha na wala halishwi? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu. Na wala usijekuwa kabisa miongoni mwa washirikina.  [Al-An’aam (6):14]

 

 

غَافِرُ الذَّنبِ

Mwenye Kughufuria Dhambi

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

غَافِرِ الذَّنبِ وَقَابِلِ التَّوْبِ شَدِيدِ الْعِقَابِ ذِي الطَّوْلِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ إِلَيْهِ الْمَصِيرُ﴿٣﴾

Mwenye kughufuria dhambi, Anayepokea tawbah, Mkali wa kuakibu, Mwenye wingi wa Ukarimu, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake ndio mahali pa kuishia.  [Ghaafir (40): 3]

 

 

 

 

إِلَـٰهِ النَّاسِ

Muabudiwa Wa Haki Wa Watu

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

إِلَـٰهِ النَّاسِ ﴿٣﴾

Muabudiwa wa haki wa watu.  [An-Naas (114): 3]

 

 

 

 

خَيْرُ الْفَاصِلِينَ

Mbora Wa Wenye Kuamua Hukumu

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قُلْ إِنِّي عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَكَذَّبْتُم بِهِ ۚ مَا عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ ۚ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۖ يَقُصُّ الْحَقَّ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الْفَاصِلِينَ ﴿٥٧﴾

Sema: Hakika mimi niko juu ya hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu nanyi mumeikadhibisha. Sina yale mnayoyahimiza. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah Pekee. Anasimulia ya haki; Naye ni Mbora wa wenye kuamua hukumu. [Al-An’aam (6): 57]

 

 

 

خَيْرُ الْفَاتِحِينَ

Mbora Wa Wenye Kuhukumu

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قَدِ افْتَرَيْنَا عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا إِنْ عُدْنَا فِي مِلَّتِكُم بَعْدَ إِذْ نَجَّانَا اللَّـهُ مِنْهَا ۚ وَمَا يَكُونُ لَنَا أَن نَّعُودَ فِيهَا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّنَا ۚ وَسِعَ رَبُّنَا كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ۚ عَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْنَا ۚ رَبَّنَا افْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِالْحَقِّ وَأَنتَ خَيْرُ الْفَاتِحِينَ ﴿٨٩﴾

Kwa yakini itakuwa tumemtungia Allaah uongo ikiwa tutarudi katika millah yenu baada ya Allaah kutuokoa nayo. Na haiwi kwetu kurejea humo isipokuwa Akitaka Allaah Rabb wetu. Rabb wetu Amekienea kila kitu kwa ujuzi. Kwa Allaah tunatawakali. Rabb wetu! Hukumu baina yetu na baina ya kaumu yetu kwa haki, Nawe ni Mbora wa wenye kuhukumu. [Al-A’raaf (7): 89]

 

 

 

 

خَيْرُ الْغَافِرِينَ

Mbora Wa Wenye Kughufuria

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَاخْتَارَ مُوسَىٰ قَوْمَهُ سَبْعِينَ رَجُلًا لِّمِيقَاتِنَا ۖ فَلَمَّا أَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ قَالَ رَبِّ لَوْ شِئْتَ أَهْلَكْتَهُم مِّن قَبْلُ وَإِيَّايَ ۖ أَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ السُّفَهَاءُ مِنَّا ۖ إِنْ هِيَ إِلَّا فِتْنَتُكَ تُضِلُّ بِهَا مَن تَشَاءُ وَتَهْدِي مَن تَشَاءُ ۖ أَنتَ وَلِيُّنَا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۖ وَأَنتَ خَيْرُ الْغَافِرِينَ ﴿١٥٥﴾

  Na Muwsaa akachagua wanaume sabini wa kaumu yake kwa ajili ya miadi Yetu kukutana kwa wakati na mahali. Kisha ilipowachukua tetemeko la ardhi; Muwsaa alisema: Rabb wangu! Ungelitaka Ungeliwaangamiza wao na mimi kabla. Je, Unatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wapumbavu miongoni mwetu?  Haya si chochote isipokuwa ni majaribio Yako. Unampotoa kwayo Umtakaye, na Unamuongoa Umtakaye. Wewe ni Mlinzi wetu, basi Tughufurie na Turehemu; Nawe ni Mbora wa wenye kughufuria. [Al-A’raaf (7): 55]

 

 

 

 

خَيْرٌ حَافِظًا

Mbora Wa Wenye Kuhifadhi

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قَالَ هَلْ آمَنُكُمْ عَلَيْهِ إِلَّا كَمَا أَمِنتُكُمْ عَلَىٰ أَخِيهِ مِن قَبْلُ ۖ فَاللَّـهُ خَيْرٌ حَافِظًا ۖ وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿٦٤﴾

 Akasema: Je, nimwaminishe kwenu ila kama nilivyokuaminini juu ya kaka yake kabla? Basi Allaah ni Mbora wa wenye kuhifadhi. Naye ni Mbora zaidi wa kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu. [Yusuf (2): 64]

 

 

خَيْرُ الْحَاكِمِينَ

Mbora Wa Wenye Kuhukumu

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَإِن كَانَ طَائِفَةٌ مِّنكُمْ آمَنُوا بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ وَطَائِفَةٌ لَّمْ يُؤْمِنُوا فَاصْبِرُوا حَتَّىٰ يَحْكُمَ اللَّـهُ بَيْنَنَا ۚ وَهُوَ خَيْرُ الْحَاكِمِينَ ﴿٨٧﴾

Na kama liko kundi miongoni mwenu limeamini kwa yale niliyotumwa nayo na kundi halikuamini; basi subirini mpaka Allaah Ahukumu baina yetu. Naye ni Mbora wa wenye kuhukumu. [Al-A’raaf (7): 87]

 

 

 

 

خَيْرُ الْمَاكِرِينَ

Mbora Wa Wenye Kupanga Makri (Njama)

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَإِذْ يَمْكُرُ بِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِيُثْبِتُوكَ أَوْ يَقْتُلُوكَ أَوْ يُخْرِجُوكَ ۚ وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ﴿٣٠﴾

Na pindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) walipokupangia makri wale waliokufuru ili wakufunge, au wakuue, au wakutoe (Makkah). Na wanapanga makri, na Allaah Anapanga makri (kupindua njama zao), na Allaah ni Mbora wa wenye kupanga makri. [Al-Anfaal (8): 30]

 

 

 

 

خَيْرُ الْمُنزِلِينَ

Mbora Wa Wenye Kuteremsha (Ardhini)

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَقُل رَّبِّ أَنزِلْنِي مُنزَلًا مُّبَارَكًا وَأَنتَ خَيْرُ الْمُنزِلِينَ ﴿٢٩﴾

Na sema: Rabb wangu! Niteremshe mteremko wa baraka, Nawe ni Mbora wa wenye kuteremsha. [Al-Mu-uminuwn (23): 29]

 

 

 

 

خَيْرُ النَّاصِرِينَ

Mbora Kabisa Wa Wenye Kunusuru

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

بَلِ اللَّـهُ مَوْلَاكُمْ ۖ وَهُوَ خَيْرُ النَّاصِرِينَ ﴿١٥٠﴾

Bali Allaah ndio Mlinzi na Msaidizi wenu. Naye ni Mbora kabisa wa wenye kunusuru. [Aali ‘Imraan (3): 150]

 

 

 

خَيْرُ الرَّاحِمِينَ

Mbora Wa Wenye Kurehemu

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّهُ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْ عِبَادِي يَقُولُونَ رَبَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ ﴿١٠٩﴾

Hakika lilikuwa kundi miongoni mwa waja Wangu, wakisema: Rabb wetu! Tumeamini, basi Tughufurie na Uturehemu, Nawe ni Mbora wa wenye kurehemu. [Al-Mu-uminuwn (23): 109]

 

 

 

 

خَيْرُ الرَّازِقِينَ

Mbora Wa Wenye Kuruzuku

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ اللَّـهُمَّ رَبَّنَا أَنزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيدًا لِّأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً مِّنكَ ۖ وَارْزُقْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١٤﴾

Akasema ‘Iysaa mwana wa Maryam: Ee Allaah, Rabb wetu, Tuteremshie meza iliyotandazwa chakula kutoka mbinguni ili iwe kwetu ni sikukuu kwa wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu; na iwe Aayah (ishara, hoja) itokayo Kwako; basi Turuzuku; kwani Wewe ni Mbora wa wenye kuruzuku.  [Al-Maa-idah (5): 114]

 

 

خَيْرُ الْوَارِثِينَ

Mbora Wa Wenye Kurithi

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَزَكَرِيَّا إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ رَبِّ لَا تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ الْوَارِثِينَ ﴿٨٩﴾

Na Zakariyyaa alipomwita Rabb wake: Rabb wangu! Usiniache pekee; Nawe Ndiye Mbora wa wenye kurithi.  [Al-Anbiyaa (21): 89]

 

 

 

 

الْمَلِكُ الْحَقُّ

Mfalme Wa Haki

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَتَعَالَى اللَّـهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۗ وَلَا تَعْجَلْ بِالْقُرْآنِ مِن قَبْلِ أَن يُقْضَىٰ إِلَيْكَ وَحْيُهُ ۖ وَقُل رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا ﴿١١٤﴾

 Basi Ametukuka Allaah kwa ‘Uluwa, Mfalme wa haki. Na wala usiiharakize Qur-aan (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kabla haikumalizwa kufunuliwa Wahy kwako. Na sema: Rabb wangu! Nizidishie elimu. [Twaa Haa (20): 114]

 

 

 

 

مَالِكُ الْمُلْكِ

Mfalme Anayemiliki Ufalme Wote

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قُلِ اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٦﴾

Sema: Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye, na Unamtukuza Umtakaye, na Unamdhalilisha Umtakaye, khayr imo Mkononi Mwako.  Hakika Wewe juu ya kila kitu ni Muweza. [Aali ‘Imraan (3): 26]

 

 

مَلِكِ النَّاسِ

Mfalme Wa Watu

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

مَلِكِ النَّاسِ ﴿٢﴾

Mfalme wa watu. [An-Naas (114): 2]

 

 

 

 

مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ

Mfalme Wa Siku Ya Malipo

 

 

 

 Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ ﴿٤﴾

Mfalme wa siku ya malipo. [Al-Faatihah (1): 4]

 

 

 

 

نُورُ السَّمَاوَاتِ

Nuru Ya Mbingu Na Ardhi

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

اللَّـهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ مَثَلُ نُورِهِ كَمِشْكَاةٍ فِيهَا مِصْبَاحٌ ۖ الْمِصْبَاحُ فِي زُجَاجَةٍ ۖ الزُّجَاجَةُ كَأَنَّهَا كَوْكَبٌ دُرِّيٌّ يُوقَدُ مِن شَجَرَةٍ مُّبَارَكَةٍ زَيْتُونَةٍ لَّا شَرْقِيَّةٍ وَلَا غَرْبِيَّةٍ يَكَادُ زَيْتُهَا يُضِيءُ وَلَوْ لَمْ تَمْسَسْهُ نَارٌ ۚ نُّورٌ عَلَىٰ نُورٍ ۗ يَهْدِي اللَّـهُ لِنُورِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَيَضْرِبُ اللَّـهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٣٥﴾

Allaah ni Nuru ya mbingu na ardhi. Mfano wa Nuru Yake kama shubaka ndani yake mna taa yenye mwanga mkali. Taa hiyo yenye mwanga mkali iko katika (tungi la) gilasi. Gilasi hiyo ni kama kwamba nyota inayong’aa na kumeremeta, inawashwa kutokana na mti wa baraka wa zaytuni, hauko Mashariki wala Magharibi. Yanakaribia mafuta yake yang’ae japokuwa moto haujayagusa; Nuru juu ya Nuru. Allaah Anamwongoza kwa Nuru Yake Amtakaye. Na Allaah Anapiga mifano kwa watu. Na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.  [An-Nuwr (24): 35]

 

 

 

 

قَابِلِ التَّوْبِ

Anayepokea Tawbah

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

غَافِرِ الذَّنبِ وَقَابِلِ التَّوْبِ شَدِيدِ الْعِقَابِ ذِي الطَّوْلِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ إِلَيْهِ الْمَصِيرُ﴿٣﴾

Mwenye kughufuria dhambi, Anayepokea tawbah, Mkali wa kuakibu, Mwenye wingi wa Ukarimu, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake ndio mahali pa kuishia. [Ghaafir (40): 3]

 

 

 

 

رَبُّ الْعَالَمِينَ

Rabb Wa Walimwengu.

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِذْ قَالَ لَهُ رَبُّهُ أَسْلِمْ ۖ قَالَ أَسْلَمْتُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٣١﴾

Rabb wake Alipomwambia: Jisalimishe na utii (Ibraahiym) Akasema: Nimejisalimisha na kutii kwa Rabb wa walimwengu. [Al-Baqarah (2): 131]

 

 

 

رَبُّ الْعَرْشِ

Rabb Wa ‘Arsh

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَإِن تَوَلَّوْا فَقُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ﴿١٢٩﴾

Na wakikengeuka, basi sema: Amenitosheleza Allaah; Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Kwake nimetawakali. Naye ni Rabb wa ‘Arsh adhimu. [At-Tawbah (9): 129]

 

 

رَبُّ الْفَلَقِ

Rabb Wa Mapambazuko

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾

Sema: Najikinga na Rabb wa mapambazuko. [Al-Falaq (113): 1]

 

 

 

رَبّ هَـٰذَا الْبَيْتِ

Rabb Wa Nyumba Hii (Al-Ka’bah)

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَلْيَعْبُدُوا رَبَّ هَـٰذَا الْبَيْتِ ﴿٣﴾

Basi wamuabudu Rabb wa nyumba hii (Ka’bah).  [Quraysh (106): 3]

 

 

 

 

رَبُّ كُلِّ شَيْءٍ ۚ

Rabb Wa Kila Kitu

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْغِي رَبًّا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيْءٍ ۚ وَلَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ إِلَّا عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿١٦٤﴾

Sema Je, nitake ghairi ya Allaah kuwa ni Rabb na hali Yeye ni Rabb wa kila kitu? Na wala nafsi yoyote haitochuma (khayr au shari) ila ni juu yake. Na wala habebi mbebaji, mzigo (wa dhambi) wa mwengine. Kisha kwa Rabb wenu ndio marejeo yenu, Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkikhitilafiana nayo.  [Al-An’aam (6): 164]

 

 

 

 

رَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ

Rabb Wa Magharibi Mbili

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ ﴿١٧﴾

Rabb wa Mashariki mbili na Rabb wa Magharibi mbili. [Ar-Rahman (55): 17]

 

 

 

رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ

Rabb Wa Mashariki Mbili

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ ﴿١٧﴾

Rabb wa Mashariki mbili na Rabb wa Magharibi mbili. [Ar-Rahman (55): 17]

 

 

 

 

رَبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ

Rabb Wa Mashariki Na Magharibi

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قَالَ رَبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٢٨﴾

 (Muwsaa) Akasema: Rabb wa Mashariki na Magharibi na vilivyo baina yake, mkiwa nyinyi ni wenye kutia akilini. [Ash-Shu’araa (26): 28]

 

 

 

 

رَبُّ النَّاسِ

Rabb Wa Watu

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾

Sema: Najikinga na Rabb wa watu.  [An-Naas (114): 1]

 

 

 

 

رَبُّ الْعِزَّةِ

Rabb Mtukufu

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٨٠﴾

Subhaana Rabbika! Utakasifu ni wa Rabb wako, Rabb Mtukufu kutokana na yale wanayoyavumisha. [Asw-Swaffaat (37): 180]

 

 

 

 

رَّبُّ السَّمَاوَاتِ السَّبْعِ

Rabb Wa Mbingu Saba

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قُلْ مَن رَّبُّ السَّمَاوَاتِ السَّبْعِ وَرَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ ﴿٨٦﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nani Rabb wa mbingu saba, na Rabb wa ‘Arsh adhimu[Al-Mu-umin (23): 86]

 

 

 

 

رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

Rabb Wa Mbingu Na Ardhi

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قُلْ مَن رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ قُلِ اللَّـهُ ۚ قُلْ أَفَاتَّخَذْتُم مِّن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ لَا يَمْلِكُونَ لِأَنفُسِهِمْ نَفْعًا وَلَا ضَرًّا ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ أَمْ هَلْ تَسْتَوِي الظُّلُمَاتُ وَالنُّورُ ۗ أَمْ جَعَلُوا لِلَّـهِ شُرَكَاءَ خَلَقُوا كَخَلْقِهِ فَتَشَابَهَ الْخَلْقُ عَلَيْهِمْ ۚ قُلِ اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿١٦﴾

Sema: Ni nani Rabb wa mbingu na ardhi? Sema: Ni Allaah. Sema: Je, mnawafanya wengineo badala Yake kuwa walinzi na hali hawamiliki kwa ajili ya nafsi zao manufaa wala dhara? Sema: Je, kipofu analingana sawa na mwenye kuona, au je, viza vinalingana sawa na nuru? Au wamemfanyia Allaah washirika walioumba kama uumbaji Wake, kisha yakafanana maumbile kwao?  Sema: Allaah ni Muumbaji wa kila kitu, Naye ni Mmoja Pekee, Asiyepingika. [Ar-Ra’d (13): 16]

 

 

 

 

رَبُّ الشِّعْرَىٰ

Rabb Wa Nyota Ya Ash-Shi’-raa

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَأَنَّهُ هُوَ رَبُّ الشِّعْرَىٰ ﴿٤٩﴾

Na kwamba Yeye ndiye Rabb wa nyota ya Ash-Shi’-raa (inayoabudiwa). [An-NAjm (53): 49]

 

 

 

 

رَفِيعُ الدَّرَجَاتِ

Mwenye Uluwa Juu Ya Vyeo Na Daraja

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

رَفِيعُ الدَّرَجَاتِ ذُو الْعَرْشِ يُلْقِي الرُّوحَ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ لِيُنذِرَ يَوْمَ التَّلَاقِ﴿١٥﴾

 (Allaah) Mwenye uluwa juu ya vyeo na daraja. Mwenye ‘Arsh, Anapelekea Ar-Ruwh (Wahy) kwa amri Yake kwa Amtakaye miongoni mwa waja Wake, ili aonye Siku ya kukutana. [Ghaafir (40): 15]

 

 

 

 

سَرِيعُ الْحِسَابِ

Mwepesi Wa Kuhesabu

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ ۗ وَمَا اخْتَلَفَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِآيَاتِ اللَّـهِ فَإِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٩﴾

Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu. Na hawakukhitilafiana wale waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia elimu kwa kufanyiana baghi na uhusuda baina yao. Na atakayekanusha Aayaat za Allaah basi hakika Allaah ni Mwepesi wa kuhesabu. [Aali ‘Imraan (3): 19]

 

 

 

شَدِيدُ الْعَذَابِ

Mkali Wa Kuadhibu

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُوا إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ الْقُوَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا وَأَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ ﴿١٦٥﴾

Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah na kuwafanya kuwa ni wanaolingana (na Allaah) wanawapenda kama kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. Na lau wangelitambua wale waliodhulumu watakapoona adhabu kwamba nguvu zote ni za Allaah; na kwamba hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu.  [Al-Baqarah (2): 165]

 

 

شَدِيدُ الْعِقَابِ

Mkali Wa Kuakibu (Kuadhibu)

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

غَافِرِ الذَّنبِ وَقَابِلِ التَّوْبِ شَدِيدِ الْعِقَابِ ذِي الطَّوْلِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ إِلَيْهِ الْمَصِيرُ﴿٣﴾

Mwenye kughufuria dhambi, Anayepokea tawbah, Mkali wa kuakibu, Mwenye wingi wa Ukarimu, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake ndio mahali pa kuishia. [Ghaafir (40): 3]

 

 

 

 

سَرِيعُ الْعِقَابِ

Mwepesi wa kuakibu (kuadhibu)

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَهُوَ الَّذِي جَعَلَكُمْ خَلَائِفَ الْأَرْضِ وَرَفَعَ بَعْضَكُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِّيَبْلُوَكُمْ فِي مَا آتَاكُمْ ۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ الْعِقَابِ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٦٥﴾

Naye (Allaah) Ndiye Aliyekufanyeni makhalifa wa duniani na Akanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja mbali mbali ili Akujaribuni katika yale Aliyokupeni. Hakika Rabb wako ni Mwepesi wa kuakibu, na hakika Yeye bila shaka ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.  [Al-An’aam (6): 165]

 

 

 

شَدِيدُ الْمِحَالِ

Mkali Na Mwenye Nguvu Za Kuhujumu

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَيُسَبِّحُ الرَّعْدُ بِحَمْدِهِ وَالْمَلَائِكَةُ مِنْ خِيفَتِهِ وَيُرْسِلُ الصَّوَاعِقَ فَيُصِيبُ بِهَا مَن يَشَاءُ وَهُمْ يُجَادِلُونَ فِي اللَّـهِ وَهُوَ شَدِيدُ الْمِحَالِ ﴿١٣﴾

Na radi inamsabihi (Allaah) kwa Himidi Zake na Malaika pia kwa kumkhofu, na Anatuma mingurumo ya radi, humsibu kwayo Amtakaye nao huku (makafiri) wakiwa wanabishana kuhusu Allaah Naye ni Mkali na Mwenye nguvu za kuhujumu. [Ar-Ra’d (13): 13]

 

 

 

سَمِيعُ الدُّعَاء

Mwenye Kusikia Du’aa

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ ۖ قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٨﴾

Hapo hapo Zakariyyaa akamwomba Rabb wake, akasema: Rabb wangu Nitunukie kutoka Kwako kizazi chema hakika Wewe ni Mwenye kusikia du’aa yangu.  [Aali ‘Imraan (3): 38]

 

 

 

وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ

Mkunjufu Wa Kughufuria

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلَّا اللَّمَمَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ ۚ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَإِذْ أَنتُمْ أَجِنَّةٌ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ ۖ فَلَا تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ ﴿٣٢﴾

Wale wanaojiepusha na madhambi makubwa na machafu isipokuwa makosa madogo-madogo. Hakika Rabb wako ni Mkunjufu wa kughufuria. Yeye Anakujueni vyema, tangu Alipokuanzisheni kutoka katika ardhi, na pale mlipokuwa mimba changa matumboni mwa mama zenu. Basi msizitakase nafsi zenu. Yeye Anamjua zaidi aliyekuwa na taqwa. [An-Najm (53): 32]

 

 

 

 

مُحْيِي الْمَوْتَى

Mwenye Kuhuisha Wafu

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَانظُرْ إِلَىٰ آثَارِ رَحْمَتِ اللَّـهِ كَيْفَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٥٠﴾

Basi tazama athari za rahmah ya Allaah vipi Anaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Hakika (Afanyayo) hayo, Ndiye bila shaka Mwenye Kuhuisha wafu, Naye juu ya kila kitu ni Muweza.  [Rum (30): 50]

 

 

 

Share