04-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: Onyo Dhidi Ya Tafsiri Ya Majina Na Sifa Za Allaah Kwa Namna Ya Kitamathali
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
04-Onyo Dhidi Ya Tafsiri Ya Majina Na Sifa Za Allaah Kwa Namna Ya Kitamathali
Imaam ‘Aliy bin Al-Murtadhwaa Al-Yamaaniy amesema:
“… Jambo la pili ni kuilaumu Dini kuwa ina ila kwa kukataa vitabu na kueleza Sifa nje nje (dhwawaahir), na kuziondoa mbali na maana zake uhakika na halisi na kuzifanya kitamathili pasi na ushahidi wa wazi na wa kauli moja ambao ungeonyesha ulazima wa taawiyl (taawili: kuipa maana ndogo, kugeuza maana halisi)). Katika hili, wanaofanya haya wanafuata Ahlul-Kalaam (watu wa balagha na kimantiki) kibubusa tu katika kanuni ambazo wao wenyewe hawajaafikiana. Baya kabisa katika haya ni madh-hab ya Qaraamitwah, Baatwiniyyah, katika taawiyl ya Majina Mazuri ya Allaah na ukanushaji wao chini ya kisingizio cha kumwepusha Allaah dhidi ya za Sifa za zinazowahusu wanaadamu tu na hivyo kuishadidisha au kuithibitsha tawhiyd machoni mwao, kwa madai ya kuyatumia Majina hayo kwa Allaah kuwa ni tashbiyh (kushabihi na wanaadamu). Haya yalifikia hatua ya kusema kuwa Yeye Hayupo, Hapatikani na Hana Sifa ya kutokuwepo au kukosekana…”
Kutokana na masuala muhimu ya Dini hii ni kuchukua Majina Mazuri ya Allaah yaliyotajwa katika Kitabu Chake kwa njia ya kumtukuza na kumsifu Yeye. Huoni kwa mfano, Ar-Rahmaan na Ar-Rahiym, husomwa katika kila Swalaah na kutajwa katika kila mjumuiko wa Kiislamu, wote wakiwa wameafikiana kuwa Majina haya mawili ni katika namna bora zaidi za kumsifu Allaah (عز وجل), na kujiweka karibu Naye kwa njia ya kumtukuza kwa majina hayo…?
Hivyo ni nini cha kuzuia kuthibitisha Sifa ya Rahmah na mfano wake zilizothibitishwa na Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) katika namna ile ile, ikiambatanishwa na kukanusha mapungufu yaliyohusiana na sifa za viumbe? Kuna kitu gani chenye kuweza kuzuia kufanywa namna kama hiyo kwa kila sifa ya Rabb ambayo pia viumbe wanayo? Yeye (سبحانه وتعالى) Amesifika nazo katika hali ya ukamilifu mkubwa zaidi, zimeondolewa namna yoyote ya ila, ilhali mja anasifika nazo huku kukiwa na ila na udhaifu. Ni katika hali hii ndipo Ahlus-Sunnah wameelewa ukanushaji wa tashbiyh, si kwa kukanusha Sifa kama wafanyavyo wenye kukanusha Sifa Zake (Mu‘atwilah).
Kutoka katika masuala yanayoashiria kutokuwa na maana taawiyl (taawili: kuipa maana ndogo, kugeuza maana halisi)), ni kuwa Mu’tazilah hawapendi ta’wiyl ambazo kundi la Ash‘ariy wanazotoa za Mwenye Hikma wa Yote Daima (Al-Hakiym). Kundi la Ash‘ariy hawapendi ta’wiyl ambazo baadhi ya Mu’tazilah hutoa za Mwenye Kusikia Yote Daima (As-Sami’) na Mwenye Kuona Yote Daima (Al-Baswiyr). Ahlus-Sunnah hawapendi taawiyl kuwa makundi yote mawili hufanya Ar-Rahmaan, Ar-Rahiym na mfano wao. Makundi yote haya hayapendi taawiyl zilizotolewa na Qaraamitwah. Hivyo ni wajibu kukazia Alichokithibitisha Allaah (عز وجل) kwa Nafsi Yake Tukufu pasi na taawiyl (kuipa maana ndogo, kugeuza maana halisi) na ta’twiyl (kuzipinga, kukanusha uwezekano).
Rai kuwa kuthibitisha maana halisi ya Majina haya ni kufuru na upotovu, kuwa Swahaba na Salaf wema hawakufahamu maana zake, au kuwa walifahamu lakini hawakubeba jukumu la kuwashauri watu juu ya maana zake halisi, haiwezekani kwa sababu ya mambo mawili:
i-Hoja muhimu na ya kauli moja kuwa asili ya mwanadamu inaeleza kuwa kila jambo la aina hii kama lingekuwa na tahadhari dhidi yake kutokea kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba wake, na lingekuwa lenye kujirudiarudia na kubwa sana kuliko tahadhari dhidi ya mwongo Dajjaal. Hilo haliwezekani kwasababu ya akili zao timamu na Dini kamilifu kuwa vipi waweze kuwaacha vizazi vyao, wake zao na jamii kwa ujumla wasikilize jambo lililohusika na Allaah ambalo maana yake halisi ni kufuru, na wakalinyamazia? Kama wangeacha tahadhari hii, kwa hakika wao wangeacha tahadhari dhidi ya Dajjaal, kwa ajili ya kutangua ubwana wake ni jambo kubwa na kalifu zaidi kiakili.
Huoni kuwa pale wale waliopewa Balagha ya Kimadhehebu (Mutakallimiyn) walipoamini mgongano wa maana halisi ya maandiko haya, tahadhari zao dhidi yake zilikuja kuwa mara nyingi kama zilivyofanya taawiyl zao kwa ajili yake? Waliandika majalada mengi kuhusu hili, waliamsha uzembe wao, walifundisha ujinga, walitangaza kufuru ya waliowapinga, na walilieneza hilo baina ya Waislamu, bali ulimwengu mzima. Hata hivyo, hili lingekuwa na haki zaidi kwa (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye ni Sayyid wa Manabii, Mtangulizi wa Salaf na wasaidizi wa Dini, kama madai yao kweli yalikuwa sahihi.
ii-Imethibitika kuwa nyongeza yoyote katika Dini imeharamishwa, hivyo si sahihi kuwa Shariy’ah iwe kimya kuhusu jambo linalotakiwa kutoka katika andiko linalotokana na misingi ya Dini. Uislamu unapaswa ufuatwe, sio uwe wa kubuni na hii ndiyo sababu unatangaza kuwa yeyote anayekana nguzo za Dini kuwa ni kafiri kwa sababu zinajulikana kwa umuhimu. Kwa hivyo, inastahiki na kufaa zaidi kuwa Shairy’ah haikuleta jambo lenye kurudiwarudiwa, kusomwa kijuujuu kuwa ni batili, lakini bila kututahadharisha nalo, hususan pindi liliposikika kuwa ni batili na linajulikana katika Vitabu vya Allaah (سبحانه وتعالى). Kwa kuhitimisha, hakuna kitukiacho kinachoweza kupingana na maana halisi ya maandiko kwa njia ya Shariy’ah au akili na hivyo kulazimika taawiyl.
Ar-Raaziy alithibitisha katika kitabu chake, Al-Arba‘iyn, naye ni alikuwa katika wapinzani wakubwa wa Ahlus-Sunnah, kuwa Vitabu vyote vya Kimbinguni vimekuja na utajo wa Sifa za Allaah, na Allaah Hakutaja andiko hata moja kuwa inatakiwa Yeye Aondolewe na Sifa ya Rahmah, Kuvumilia, Hikma na mfano wake. Hivyo suala hili liko dhahiri ingawa anaweza kukataa.[1]
[1] Iythaar Al-Haqq ‘Alal-Khalq (uk. 219 +) ya Al-Yamaniy pamoja na mukhtasari, kama kilivyonukuliwa katika Sharh Kitaab At-Tawhid min Swahiyh Al-Bukhaariy (1/86+) cha Shaykh ‘Abdullah Al-Ghunaymaan.