06-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الرَّب
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الرّب
Idadi kubwa ya Majina Mazuri na Kamilifu ya Allaah (عز وجل) yamerudiwarudiwa mara kadhaa katika Qur-aan kama matukio yalivyohitaji, na kuna ulazima wa kuelezea maana zake kwa ufupi na ya kufahamika. Hivyo tunasema:
الرّب Ar-Rabb:
Rabb Wa Kila Kitu, Mlezi, Mola, Bwana, Muumbaji, Msimamizi, Mneemeshaji, Mfalme, Mwenye Kuruzuku, Mwendeshaji wa Mambo
|
Jina hili limerudiwarudiwa katika Aayah nyingi.
Allaah (سبحانه وتعالى) – Ni Ar-Rabb Ambaye Anayelea na kukimu waja Wake kwa kuendesha na kusimamia mambo yao yote na kuwapa namna zote za fadhila na baraka. Hususan kabisa, Yeye Ndiye Anayelea na kukimu marafiki wa waja wanyoofu kwa kusahihisha na kutakasa nyoyo, roho na maadili yao. Kwa ajili hii, du’aa zao mara kwa mara huombwa kwa Jina hili tukufu kwasababu wanatafuta malezi haya hasa.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَرَبُّكَ الْغَفُورُ ذُو الرَّحْمَةِ ۖ لَوْ يُؤَاخِذُهُم بِمَا كَسَبُوا لَعَجَّلَ لَهُمُ الْعَذَابَ ۚ بَل لَّهُم مَّوْعِدٌ لَّن يَجِدُوا مِن دُونِهِ مَوْئِلًا ﴿٥٨﴾
Na Rabb wako ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye Rahmah. Kama Angeliwachukulia kwa yale waliyoyachuma, Angeliwaharakizia adhabu. Bali wao wana miadi, hawatopata pasi Naye kimbilio la kuepukana nayo. [Al-Kahf (18): 58]