07-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الله
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الله
الله Allaah Mwenye Uluwhiyyah, Mwenye ‘Ubuwdiyyah
|
Allaah (سبحانه وتعالى) ni Ilaah Mmoja Pekee Ambaye Ndiye Anayeabudiwa na Ndiye mwenye haki ya kuabudiwa na viumbe wake wote. Hayo ni kwasababu ya sifa nzuri na kamilifu za Ki Ilaah Alizo Nazo Yeye:
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾
Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kufikia kuelewa chochote kuhusu ujuzi Wake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye Uluwa; Ametukuka, Adhimu; Mkuu kabisa. [Al-Baqarah (2): 255]