16-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْحَمِيدُ
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الْحَمِيدُ
الْحَمِيدُ Al-Hamiyd Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa
|
Allaah (عز وجل), Katika Nafsi Yake, Majina Yake, Sifa Zake na Matendo Yake. Ana Majina bora kuliko wote, na Ana Sifa kamilifu zaidi kuliko wote zikiambatana na matendo bora na timilifu kuliko wote.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
الر ۚ كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ ﴿١﴾
Alif Laam Raa. Kitabu Tumekiteremsha kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili uwatoe watu kutoka kwenye viza kuwaingiza katika nuru kwa idhini ya Rabb wao, waelekee katika njia ya Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote. [Ibraahiym (14): 1]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَقَدْ آتَيْنَا لُقْمَانَ الْحِكْمَةَ أَنِ اشْكُرْ لِلَّـهِ ۚ وَمَن يَشْكُرْ فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿١٢﴾
Kwa yakini Tulimpa Luqmaan hikmah kwamba: Mshukuru Allaah. Na anayeshukuru, basi hakika anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na anayekufuru, basi hakika Allaah ni Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote. [Luqmaan (31): 12]