17-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْمَجِيدُ - الْكَبِيرُ - الْعَظِيمُ - الْجَلِيلُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْمَجِيدُ - الْكَبِيرُ - الْعَظِيمُ - الْجَلِيلُ

 

 

الْمَجِيدُ

Al-Majiyd

Mwingi Mno Wa Vipawa Na Ukarimu

 

 

الْكَبِيرُ

Al-Kabiyr

Mkubwa Wa Dhati, Vitendo Na Sifa

 

 

الْعَظِيمُ

Al-‘Adhwiym

Adhimu, Mwenye Taadhima

 

 

الْجَلِيلُ

Al-Jaliyl

Jalali, Mwenye Ujalali, Mtukuka Daima, Mwenye Hadhi

 

 

 

Allaah (عز وجل), Yeye Ana Aifa ya ‘Uluwa, Utukufu na Ukubwa. Yeye Ndiye mkubwa kuliko wote, Mtukuka zaidi na mkubwa kuliko kitu chochote. Yeye Huadhimishwa na kufanywa mkubwa nyonyoni mwa marafiki zake na walio karibu Naye, nyoyo zao zinatiririkiwa na ukubwa Wake na taadhima Yake, kujisalimisha mbele Yake na unyenyekevu mbele ya utukufu Yake.

 

Anasema Allaah (عز وجل):

ذُو الْعَرْشِ الْمَجِيدُ ﴿١٥﴾

Mwenye ‘Arsh; Mwenye utukufu kamili, enzi, wingi wa vipawa, fadhila na ukarimu. [Al-Buruwj (85):15]

 

Na Anasema pia Allaah (عز وجل):

عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْكَبِيرُ الْمُتَعَالِ ﴿٩﴾

Mjuzi wa ghayb na dhahiri, Mkubwa wa dhati vitendo na sifa, Mwenye Uluwa Aliyejitukuza kabisa. [Ar-Ra’d (13): 9]

 

Na pia Anasema Allaah (عز وجل):

 

فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ ﴿٧٤﴾

Basi sabbih kwa Jina la Rabb wako Adhimu Mkuu kabisa. [Al-Waaqi’ah (56): 74]

 

 

 

 

 

Share