18-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْعَفُوُّ - الْغَفُورُ - الْغَفَّارُ
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الْعَفُوُّ - الْغَفُورُ - الْغَفَّارُ
الْعَفُوُّ Al-‘Afuww Mwingi Wa Kusamehe
|
الْغَفُورُ Al-Ghafuur Mwingi Wa Kughufiria, Kusitiri
|
الْغَفَّارُ Al-Ghaffaar Mwingi Wa Kughufuria, Kusitiri Mara Kwa Mara
|
Allaah (عز وجل) ni Pekee Ambaye Alikuwa na hata sasa ni Mwenye Sifa ya kusamehe. Allaah (عز وجل) Ndiye Aliyekuwa, na hata sasa Anaonyesha msamaha na huruma kwa waja Wake. Kila mmoja yuko katika haja kubwa sana ya maghfirah Yake kama walivyo na haja kubwa ya Rahmah Yake na ukarimu. Allaah (سبحانه وتعالى) Ameahidi maghfirah na msamaha kwa mwenye kutimiza masharti yake.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَإِنِّي لَغَفَّارٌ لِّمَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا ثُمَّ اهْتَدَىٰ ﴿٨٢﴾
Na hakika Mimi bila shaka ni Mwingi mno wa kughufuria kwa anayetubia na akaamini na akatenda mema kisha akaendelea kuongoka. [Twahaa (20): 82]
Na pia Anasema Allaah (عز وجل):
دَرَجَاتٍ مِّنْهُ وَمَغْفِرَةً وَرَحْمَةً ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٩٦﴾
Ni daraja za vyeo (vya juu) kutoka Kwake na maghfirah na rahmah. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [An-Nisaa (4): 96]
Na pia Anasema Allaah (عز وجل):
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ إِنِ افْتَرَيْتُهُ فَلَا تَمْلِكُونَ لِي مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَا تُفِيضُونَ فِيهِ ۖ كَفَىٰ بِهِ شَهِيدًا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۖ وَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٨﴾
Je, wanasema ameitunga? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ikiwa nimeitunga, basi hamna uwezo wa kunifaa chochote mbele ya Allaah. Yeye Anajua zaidi yale mnayoyaropokwa. Ananitosheleza kuwa Shahidi baina yangu na baina yenu; Naye Ndiye Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Ahqaaf (46): 8]
Na pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى) :
إِن تُبْدُوا خَيْرًا أَوْ تُخْفُوهُ أَوْ تَعْفُوا عَن سُوءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا قَدِيرًا ﴿١٤٩﴾
Mkidhihirisha khayr au mkiificha au mkisamehe uovu; basi hakika Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Muweza wa yote. [An-Nisaa (4): 149]