21-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْعَلِيُّ - الأَعْلى
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الْعَلِيُّ - الأَعْلى
الْعَلِيُّ Al‘Aliyy Yuko Juu Ya Vyote, Mwenye ‘Uluwa
|
الأَعْلى Al-A’laa Mwenye ‘Uluwa Na Taadhima Kuliko Vyote
|
Allaah (سبحانه وتعالى), Kwake Yeye ndipo kwenye ‘Uluwa katika vipengele Vyake vyote. ‘Uluwa wa Nafsi Yake, ‘Uluwa wa Sifa Zake na enzi, ‘Uluwa wa nguvu na nguvu. Allaah (عز وجل), Yeye Ndiye Pekee aliye katika Kiti Chake cha Enzi na Ndiye Aliyekizunguka kwa mamlaka. Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Pekee ambaye ziko Kwake Sifa za ukubwa, utukufu, ukuu na uzuri unapata ukamilifu na utimilifu.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ﴿٤﴾
Ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, Naye ni (Mwenye ‘Uluwa, Ametukuka, Mwenye Taadhima, Mkuu kabisa. [Ash-Shuwraa (42): 4]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى ﴿١﴾
Sabbih Jina la Rabb wako Mwenye ‘Uluwa Ametukuka kabisa kuliko vyote. [Al-A’laa [(87): 1]