22-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْعَزِيزُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْعَزِيزُ

 

 

الْعَزِيزُ

Al-‘Aziyz

Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika Daima

 

 

 

Allaah (عز وجل) ni Pekee Aambaye Kwake ndiko kwenye nguvu na taadhima katika ukamilifu Wake, nguvu na taadhima ya nguvu, ya ushindi na ya kuzuia. Amewazuia viumbe Wake wote dhidi ya kumzunguka na kumkamata. Allaah (عز وجل), Yeye ni Mweza  juu ya kila kitu kilichopo, viumbe wote ni watawaliwa na wanawajibika Kwake, wamesalimu amri mbele ya Utukufu Wake.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَلَهُ الْكِبْرِيَاءُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٣٧﴾

Na Ukubwa, Uadhama, Ujalali ni Wake Pekee mbinguni na ardhini; Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [AL-Jaathiyah (45): 37]

Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿١﴾

Amebarikika Ambaye Mkononi Mwake umo ufalme Naye juu ya kila kitu ni Muweza.

 

الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْغَفُورُ﴿٢﴾

Ambaye Ameumba mauti na uhai ili Akujaribuni ni nani kati yenu mwenye ‘amali nzuri zaidi. Naye ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwingi wa kughufuria. [Al-Mulk (67): 1-2]

 

 

 

 

Share