23-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْقَوِيُّ - الْمَتِينُ
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الْقَوِيُّ - الْمَتِينُ
الْقَوِيُّ Al-Qawiyy Mwenye Nguvu
|
الْمَتِينُ Al-Matiyn: Mwenye Nguvu Na Shadidi, Madhubuti
|
Majina haya yanaingia katika maana ya Al’Aziyz.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِم بِغَيْرِ حَقٍّ إِلَّا أَن يَقُولُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ۗ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّـهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّهُدِّمَتْ صَوَامِعُ وَبِيَعٌ وَصَلَوَاتٌ وَمَسَاجِدُ يُذْكَرُ فِيهَا اسْمُ اللَّـهِ كَثِيرًا ۗ وَلَيَنصُرَنَّ اللَّـهُ مَن يَنصُرُهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٤٠﴾
Ambao wametolewa majumbani mwao bila ya haki isipokuwa kwa kuwa wanasema: Rabb wetu ni Allaah. Na lau ingelikuwa Allaah Hawakingi watu baadhi yao kwa wengine, bila shaka yangelivunjwa mahekalu na makanisa, na masinagogi na Misikiti inayotajwa humo Jina la Allaah kwa wingi. Na bila shaka Allaah Atamnusuru yeyote yule anayenusuru Dini Yake. Hakika Allaah bila shaka ni Mwenye nguvu zote, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika. [Al-Hajj (22): 40]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ ﴿٥٨﴾
Hakika Allaah Ndiye Mwingi wa kuruzuku, Mwenye nguvu Madhubuti. [Adh-Dhaariyaat (51): 58]