24-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْجَبَّارُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْجَبَّارُ

 

 

 

 

الْجَبَّارُ

Al-Jabbaar

Jabari, Mwenye Kulazimisha, Mwenye Kuunga

 

 

 

 

Jina hili la Allaah (سبحانه وتعالى)  linajumuisha maana ya Al-‘Aliy na Al-A’laa, maana ya Al-Qahhaar na maana ya Ar-Rauwf.

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayezifanyia ukarimu na kuziponya roho. Allaahz ni Pekee Anayewapa nguvu wanyonge na walio dhaifu, Allaah (عز وجل) ni Pekee Anayewalinda na kuwapa hifadhi wale wanaokimbilia Kwake na kuomba hifadhi Kwake.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٢٣﴾

Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mfalme, Mtakatifu Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye kusalimisha na Amesalimika na kasoro zote, Mwenye kusadikisha ahadi na kuaminisha, Mwenye kudhibiti, kushuhudia, kuchunga na kuhifadhi, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Jabari, Asiyeshindwa kufanya Atakalo, Mwenye ukubwa na uadhama, Subhaana Allaah! Utakasifu ni wa Allaah kutokana na ambayo wanamshirikisha. [Al-Hashr (59): 23]

 

 

 

 

Share