35-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْقَهَّارُ - الْقَاهِرُ
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الْقَهَّارُ - الْقَاهِرُ
الْقَهَّارُ Al Qahhaar Mwenye Kuteza Nguvu Asiyepingika
|
الْقَاهِرُ Al-Qaahir Mwenye Kuteza Nguvu Asiyepingika
|
Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Aliyekitiisha kila kitu. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Ambaye mbele Yake uumbaji wote umetii na kunyenyekea mbele ya utukufu na nguvu kamilifu.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۖ وَيُرْسِلُ عَلَيْكُمْ حَفَظَةً حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ ﴿٦١﴾
Naye ni Asiyepingika, Aliye Mkuu kabisa juu ya waja Wake, na Anakutumieni Malaika wanaohifadhi hata yanapomfikia mmoja wenu mauti, Wajumbe Wetu humfisha, nao hawafanyi taksiri. [Al-An’aam (6): 61]
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
فَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّـهَ مُخْلِفَ وَعْدِهِ رُسُلَهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٤٧﴾
Basi usidhanie kwamba Allaah ni Mwenye kukhalifu ahadi Yake kwa Rusuli Wake. Hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kulipiza.
يَوْمَ تُبَدَّلُ الْأَرْضُ غَيْرَ الْأَرْضِ وَالسَّمَاوَاتُ ۖ وَبَرَزُوا لِلَّـهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ﴿٤٨﴾
Siku ardhi itakapobadilishwa kuwa ardhi nyingine na mbingu pia na (viumbe wote) watahudhuria kwa Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika. [Ibraahiym (14): 47-48]