36-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْمُقِيتُ
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الْمُقِيتُ
الْمُقِيتُ Al-Muqiyt Mwenye Kuruzuku Chakula
|
Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Ambaye hukipa riziki kila kiumbe kilichopo kwa kitu cha kukitia nguvu, Anayekipa chakula na kukiongoza kwa vyovyote Atakavyo kulingana na hikma na sifa Yake.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
مَّن يَشْفَعْ شَفَاعَةً حَسَنَةً يَكُن لَّهُ نَصِيبٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن يَشْفَعْ شَفَاعَةً سَيِّئَةً يَكُن لَّهُ كِفْلٌ مِّنْهَا ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقِيتًا ﴿٨٥﴾
Atakayeombea uombezi mzuri atapata fungu lake katika hayo. Na atakayeombea uombezi mbaya atapata sehemu yake katika hayo. Na Allaah daima ni Mwenye kudhibiti na Mwangalizi wa kila kitu. [An-Nisaa (4): 85]