47-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْقَابِضُ - الْبَاسِطُ
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الْقَابِضُ - الْبَاسِطُ
الْقَابِضُ Al-Qaabidhw Mwenye Kuchukua
|
الْبَاسِطُ Al-Basitw Mwenye Kukunjua
|
Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayetoa rizki na roho. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayeruzuku burebure na anazipa uhai nyoyo. Yote haya ni kulingana na Hikmah na Rahmah Yake.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ أَضْعَافًا كَثِيرَةً ۚ وَاللَّـهُ يَقْبِضُ وَيَبْسُطُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٤٥﴾
Ni nani atakayemkopesha Allaah mkopo mzuri kisha (Allaah) Amzidishie mzidisho mwingi. Na Allaah Anakunja na Anakunjua, na Kwake mtarejeshwa. [Al-Baqarah (2): 245]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٦٧﴾
Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria; na hali ardhi yote itatekwa Mkononi Mwake Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia. Subhaanahu wa Ta’aalaa (Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa) kutokana na yale yote wanayomshirikisha. [Az-Zumar (39): 67]