48-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْمُعْطِي - الْماَنِعُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الْمُعْطِي - الْماَنِعُ

 

 

الْمُعْطِي

Al-Mu’twiy

Mpaji

 

 

الْماَنِعُ

Al-Maani’u

Mwenye Kuzuia

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayetoa rizki na mahitaji ya waja Zake na Anayezuia. Hakuna wa kukizuia Anachokitoa na hakuna wa kikutoa Anachozuia. Kitu chochote chenye kuleta jema au manufaa hutafutwa na kutamaniwa kutoka Kwake. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Ambaye Anampa yeyote Amtakaye na kumzuia yeyote Amtakaye, yote haya kulingana na Hikmah na Rahmah yake.

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

كُلًّا نُّمِدُّ هَـٰؤُلَاءِ وَهَـٰؤُلَاءِ مِنْ عَطَاءِ رَبِّكَ ۚ وَمَا كَانَ عَطَاءُ رَبِّكَ مَحْظُورًا ﴿٢٠﴾

Wote hao Tunawakunjulia; hawa na hao katika hiba za Rabb wako. Na hazikuwa hiba za Rabb wako zenye kuzuiliwa. [Al-Israa (17): 20]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu Nabiy Sulaymaaan na du’a yake aliyoomba:

 

 

قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَهَبْ لِي مُلْكًا لَّا يَنبَغِي لِأَحَدٍ مِّن بَعْدِي ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ ﴿٣٥﴾

Akasema: Rabb wangu! Nighufurie, na Nitunukie ufalme asiupate mtu yeyote baada yangu; hakika Wewe Ndiye Mwingi Wa kutunuku.

 

فَسَخَّرْنَا لَهُ الرِّيحَ تَجْرِي بِأَمْرِهِ رُخَاءً حَيْثُ أَصَابَ ﴿٣٦﴾

Basi Tukamtiishia upepo unaokwenda kwa amri yake pole pole popote anapotaka kufika.

 

وَالشَّيَاطِينَ كُلَّ بَنَّاءٍ وَغَوَّاصٍ ﴿٣٧﴾

Na mashaytwaan, kila ajengaye na mpiga mbizi.

 

وَآخَرِينَ مُقَرَّنِينَ فِي الْأَصْفَادِ ﴿٣٨﴾

Na wengineo, wafungwao minyororoni.

 

هَـٰذَا عَطَاؤُنَا فَامْنُنْ أَوْ أَمْسِكْ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٣٩﴾

 (Tukasema) Hiki ni kipawa Chetu, basi toa au zuia bila ya hesabu. [Swaad (38): 35 - 39]

 

 

 

Share