49-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الشَّهِيدُ
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الشَّهِيدُ
الشَّهِيدُ Ash-Shahiyd Shahidi Mwenye Kujua Vyema Yenye Kuonekana Na Yasiyoonekana, Mwenye Kushuhudia
|
Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayekijua kila kitu. Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayesikia kila sauti kubwa na ya ukimya. Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayeona kila kitu kisicho muhimu na kilicho muhimu, kidogo na kikubwa. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Ambaye ‘ilmu Yake inakizunguka kila kitu. Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Atakayetoa ushahidi wa kutetea au dhidi ya waja Wake kwa yale waliyoyafanya.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
قُلْ أَيُّ شَيْءٍ أَكْبَرُ شَهَادَةً ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ شَهِيدٌ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۚ وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ ۚ أَئِنَّكُمْ لَتَشْهَدُونَ أَنَّ مَعَ اللَّـهِ آلِهَةً أُخْرَىٰ ۚ قُل لَّا أَشْهَدُ ۚ قُلْ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ وَإِنَّنِي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ ﴿١٩﴾
Sema: Kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa zaidi? Sema: Allaah; ni Mwenye kushuhudia yote baina yangu na baina yenu. Na nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia. Je, hivi nyinyi hakika mnashuhudia kwamba wako waabudiwa wengine pamoja na Allaah? Sema: Mimi sishuhudii (hayo). Sema: Hakika Yeye ni Mwabudiwa wa haki Mmoja (Pekee), na kwamba hakika mimi sihusiki na mnavyomfanyia shirki. [Al-An’aam (6): 19]
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا﴿٢٨﴾
Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote. Na Allaah Anatosha kuwa ni Shahidi. [Al-Fath (48): 28]