Vilosa
Vilosa
Vipimo
Mchele - 1/2 Kikombe
Semolin - 1 Vikombe
Tui la nazi - 3/4 Kikombe
Maziwa - 1/2 Kikombe
Mayai - 3
Hamira - 1 kijiko cha chai kijae
Rose essence - kidogo
Zaafarani - kidogo
Sukari - 1 kijiko cha chai
Namna ya kutayarisha na kutengeneza
- Roweka mchele tokea usiku
- Uchuje mchele maji yote
- Weka kwenye mashine ya kusagia (Blender)
- Tia mayai, maziwa, sukari, hamira , rose essence, zaafarani. Kasha usagesana mpaka chenga za mchele zote zisagike.
- Tia semolina na tui la nazi, kasha endelea kusaga katika blender, kidogo mpaka ichanganyike vizuri.
- Mimina katika bakuli kubwa, funika iwache iuumuke.
- Ikishaumuka choma kama unavyochoma vitumbua.
- Shira ikipowa, tumbukiza Vilosa kwa kiasi kiasi , changanya na uvitoe uviweke upande katika sahani ya kupakulia.
- Endelea kufanya mpaka vyote vimalizike.
Shira : Tengeneza mapema ipowe. Na isiwe nzito
Sukari - 2 Vikombe
Maji - 1 kikombe
Zaafarani - kidogo
Rose - Essence