Halwa - Halua
Halwa - Halua
Vipimo
Tambi za Mchele - Pakti 1 (400 mg)
Tui la nazi - Kikombe 1
Sukari - Nusu kikombe, ukipenda ongeza kidogo
Maziwa ya kopo (evaporated) - Nusu kikombe
Samli - Kijiko 1 cha supu
Zabibu kavu - ¼ Kikombe
Liki - ¼ kijiko cha chai
'Arki (rose flavour) - Matone matatu au zaidi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Roweka majani ya chai vikombe 2 vya maji ya moto upate rangi iliyokoza.
- Chuja kwenye sufuria kubwa, mimina maji lita tatu na nusu au birika ya umeme mawili ya maji.
- Kwenye hayo maji tia, sukari, iliki,maji ya majani ya chai,zafarani na arki. Wacha mpaka ichemka.
- Wakati sufuria ipo jikoni chukua kibakuli utie unga wa conflour changanya na maji ya kawaida vikombe viwili.
- Mchanganyiko ukishakuaanza kuchemka mimina ule unga uliouchanganya na maji, koroga bila kuachia mkono kwa kutumia mwiko mrefu.
- Ukiona mchanganyika umeshashikana sawa sawa, mimina samli vikombe viwili.
- Endelea kukoroga bila ya kuachia na mchanganyiko ukiwamzito tia samli na endelea kukoroga. Muda wote koroga kwa mzunguko wa kuelekea upande mmoja tu kushoto au kulia. ( clockwise au anticlockwise)
- Utaendelea kufanya hivyo kwa masaa mawili mpaka mafuta yajitenge mbali na halua. Na yataanza kuruka ruka.
- Ili kujua kama halua tayari imeshawiva, ukiwa unakoroga chota kwenye kijiko kidogo uiache ipoe, kama inaonekana ipo ngumu baada ya kupoa , basi itakuwa tayari,la nilaini sana iwache kwenye moto huku unaendelea kukoroga mpaka iwe ngumu kwenye kijiko ikipoa.
- Ikiwa tayari tenganisha mafuta yote na halua.
- Baada ya hapo itie kwenye trays au vibakuli ya ufuniko na uipambie kwa kumwagia juu lozi zilizokatwa katwa.
Kidokezo:
Unaweza kupambia lozi , njugu au ufuta juu. Pia unaweka kwenye mchanganyiko vitu hivyo pale unakoroga ikiwa ipo jikoni.