Kaimati (Aina Ya 3)
Kaimati (Aina Ya 3)
Vipimo
Unga - 2 vikombe vya chai
Hamira - 1 ½ cha chai
Samli - 1 kijiko cha chai
Maji - 1 ½ kikombe cha chai (kiasi)
Mafuta ya kukaangia - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya unga Hamira, Samli, maji, kisha vuruga kulainisha unga hadi uwe hauna madonge na mwepesi kiasi.
- Funika unga uumuke. Ukiuumuka (ukifura) choma kaimati katika mafuta ya moto.
- Ziepue na zichuje mafuta.
- Weka kaimati katika bakuli au sahani kisha mwagia *Shira zikiwa tayari.
Shira:
Sukari - 3 vikombe
Maji - 1 kikombe
Hiliki - ¼ kijiko cha chai
Arki (rose flavour) - 3-4 matone
Namna Ya Kutayarisha Shira
- Tia sukari na maji katika kisufuria kidogo, acha kwenye moto ichemke pole pole hadi iwe nzito ya kunata.
- Tia hiliki na arki ikiwa tayari kumwagiwa juu ya kaimati, huku unavichanganya na huku shira ikipowa na kugeuka kuwa sukari kavu.
Kidokezo:
Shira ya Kaimati hizi iwe nzito ili unapochanganya na kaimati igeuke kuwa kama sukari ya visheti.