Halwa/Halua Ya Karoti
Halwa/Halua Ya Karoti
Vipimo
Karoti iliyoparuzwa - 3 vikombe vya chai
Sukari - 2 vikombe vya chai
Maziwa - 2 vikombe vya chai
Lozi au korosho - 1 kikombe cha chai
zilizokatwa ndogo ndogo
Hiliki - ½ kijiko cha chai
Samli - 4 vijiko vya chai vidogo
Namna ya kutayarisha na kupika
- Kaanga lozi kwa ile samli kidogo ziweke pembeni.
- Tia maziwa, hiliki na sukari kwenye sufuria chemsha ikisha chemka mimina Karoti.
- Chemsha mpaka ikauke maziwa tia lozi.
- Mimina kwenya trei.
- Ikisha kupoa kata vipande. Tayari kwa kuliwa.
