Vipopoo/Matobosho
Vipopoo/Matobosho
Vipimo
Unga ngano - 2 na nusu kikombe
Maji - 3 kikombe
Chumvi - kijiko nusu cha chai
Mafuta - 5 kijiko cha supu
Tui la nazi la kopo - 1000 ml
Iliki iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Sukari - Kikombe nusu
Namna Ya Kutayarisha Na kupika
- Chemsha maji paka yatokote na hiyo chumvi
- Yakitokota mimina unga uache ndani kwa dakika tano.
- Songa kama ugali kwa kutumia nguvu zako na kukazanisha sufuria sawa sawa kwani ugali wake huwa mgumu si kama ugali wa kawaida.
- Ukishakuwa ugali mimina kwenye kibao au meza au sinia pana kisha ukande kidogo ukiwa umejipaka mafuta mikononi.
- Menya vijidonge usukume kwa mkono moja paka iwe bakora ndefu ima iwe nzito au nyembamba bila kutia mafuta wala unga mkavu.
- Uwanie kuufanya hizo bakora paka umalize bila kukauka .
- Zikatekate bakora kwa kisu vipande vipande ukubwa wa nusu inchi au inchi moja kama ilivyo kwenye picha.
- Kila kipande chovya mafuta kwa kidole ukibonyeza kati ili kujenga kiduwara.
- Tia tui nusu kwenye sufuria ya nafasi na iliki uzichemshe mpaka zitokote
- Mimina vitobosha vyote kweye mchemko wa tui na iliki .
- Moto mdomdogo ongeza tui lilobakia acha kwa daikika 30 kutokota.
- Tia sukari huku unakoroga koroga kuchanganya matobosha na tui.
- Yakitokota yakiwa mazito yaepue usiyaache yakakauka tui lote na uonje sukuari, ikiwa imetokeza utamu tayari kuliwa lakini mpaka yapowe ndio huwa mazuri zaidi.
Kidokezo:
Kwa wenye friji wanaweza kugawa matobosha kabla kuyapika kwa siku ya pili au ya tatu ikiwa umeyatia ndani ya mifuko ya plastiki maalum ya kuwekea vitu frijini. Lakini siku utakayodhamiria kupika basi paka uyapashe moto kwenye (microwavel) kwa sekunde 60 ili yalainike kwa kupikwa.