Ndizi Mbivu
Ndizi Mbivu
Vipimo
Ndizi Mbivu - 6
Nazi - Kikopo 1
Sukari -Vijiko 3 vya chakula
Hiliki - Kijiko 1
Namna ya kutayarisha na kupika
- Menya ndizi kisha zipasue kati utoe ule moyo wa kati.
- Zikate size unayopenda mwenyewe, kisha uzipange ndani ya sufuria.
- Weka maji kiasi na uzichemshe ndizi kidogo, karibu ya kuiva mimina tui.
- Mimina sukari na hiliki ndani ya ndizi na ziwache zichemke mpaka tui libaki kidogo.
- Ziondoe jikoni na uziweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
Kidokezo:
Ni nzuri sana kuliwa na kitu cha chumvi kama nyama ya kukausha au kuku wa kuchoma.
