Vibibi Vya Tui Na Kunyuyuziwa Zabibu
Vibibi Vya Tui Na Kunyuyuziwa Zabibu
Vipimo
Mchele vikombe 2
Unga wa ngano 1 kijiko cha kulia
Hamira kijiko 1 cha chai
Tui zito vikombe 2
Maziwa ya unga ¼ kikombe
Hiliki ½ kijiko cha chai
Sukari ½ kikombe
Samli ya kupikia
Vipimo Vya Tui La Kupakaza Juu Ya Vibibi
Tui zito la nazi 1
Unga wa ngano 1 kijiko cha supu
Sukari ½ kikombe
Maziwa mazito ½ kikombe
Hiliki ½ kijiko cha chai
Arki (rose flavour) ½ kijiko cha chai
Zabibu za kunyunyuzia kiasi
Namna Ya Kupika Tui La Vibibi
- Changanya vitu vyote katika sufuria ukoroge vizuri kisha weka katika moto huku unakoroga mpaka lichemke kiasi ya dakika chache.
- Epua likiwa tayari.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Vibibi
- Roweka mchele masaa mengi. Kisha chuja maji
- Weka mchele katika mashine ya kusagia (blender) utie tui kidogo kidogo usage mpaka ulainike vizuri.
- Tia vitu vilobakia isipokuwa samli usage tena uchanganyike. Kisha mimina katika bakuli uache uumuke.
- Weka chuma kidogo katika moto paka samli kiasi ½ kijiko cha chai, teka mchanganyiko umimine katikati.
- Kibibi kiwiva chini geuza upike upande wa pili. Endelea upange vibibi katika sahani.
- Pakaza tui lake na nunyizia zabibu. Tayari kuliwa.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)