Tende Ya Kusonga Ya Lozi Na Cornflakes
Tende Ya Kusonga Ya Lozi Na Cornflakes
Vipimo
Tende zilizotolewa kokwa - 1 Kilo
Cornflakes - 1 ½ kikombe
Lozi Zilokatwa katwa - 1 kikombe
Siagi - ¼ kilo
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Mimina tende na siagi kwenye sufuria bandika motoni moto mdogo mdogo mpaka zilainike. Kwa muda wa dakika 10.
- Isonge kidogo kwa mwiko au kuikoroga ichanganyike vizuri.
- Changanya Cornflakes na lozi kwenye tende mpaka zichanganyika vizuri.
- Pakaza treya au sinia mafuta au siagi kidogo.
- Mimina mchanganyiko wa tende, zitandaze vizuri na ukate vipande saizi unayopenda. Zikiwa tayari kuliwa kwa kahawa.