Viazi Vitamu Vya Nazi
Viazi Vitamu Vya Nazi
Vipimo
Viazi vitamu - 6 Vikubwa
Tui la nazi - 3 Vikombe
Sukari - ½ Kikombe
Hiliki - 1 Kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Menya viazi vitamu na kisha vikate vipande vipande;
- Kosha vizuri na vitie katika sufuria na uviweke jikoni;
- Vikisha wiva mimina tui la nazi kisha weka sukari na hiliki;
- Acha tui la nazi, sukari na hiliki vichemke na vichanganyike vizuri katika viazi hivyo hadi kukauka na kubaki rojo kiasi;
- Pakua tayari kuliwa.