Crapes Za Maziwa Kwa Asali
Crapes Za Maziwa Kwa Asali
Vipimo
Unga wa ngano - 1 Kikombe
Sukari - 2 Vijiko vya supu
Baking powder - 1 Kijiko cha supu
Chumvi - 1/2 Kijiko cha chai
Mayai - 2
Maziwa - 2 Vikombe
Ngano yakupikika haraka(oats) - 1 Kikombe
Siagi (iliyoyayushwa),au mafuta - 2 Vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Weka unga, sukari, baking powder na chumvi katika bakuli.
- Kwenye bakuli jengine, piga mayai kidogo changanya maziwa, ngano na siagi na iache ikae dakika mbili.
- Kisha changanya pamoja na mchanganyiko wa unga.
- Weka chuma kisichoganda (non stick) kipate moto.
- Paka mafuta kidogo kisha tumia kijiko cha kupakulia tia mchanganyiko iwe duara (kama vibibi).
- Itakapoanza kufanya mapovu juu, geuza upande wa pili hadi iive.
- Endelea hivyo hivyo mpaka umalize unga wote.
- Panga kwenye sahani na tayari kuliwa na asali au shira ya sukari pekee au shira ya matunda kama maple syrup.
Kidokezo
Unaweza kutumia chuma kikubwa kufanya viduara 3 au 4 kwa mara moja