51-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الْفَعَّالُ لِّمَا يُريدُ
Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi
(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)
الْفَعَّالُ لِّمَا يُريدُ
الْفَعَّالُ لِّمَا يُريدُ Al-Fa’aalu Limaa Yuriyd Mwenye Kufanya Atakacho
|
Allaah (سبحانه وتعالى) ni Mwenye Kufanya Atakalo. Sifa hii ni kwasababu ya ukamilifu wa nguvu Yake na utekelezaji wa utashi na amri Yake kuwa kila kitu Anachotaka kukifanya, Anakifanya na kuwa hakuna wa kumzuia au kukataa. Hana msaidizi kwa kitu chochote Anachokifanya, bali Anapotaka jambo huliambia tu:
كُن فَيَكُونُ
Kun! basi (jambo) huwa!
Licha ya ukweli kuwa Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) hufanya Atakacho, utashi Wake unatenda kulingana na Hikmah Yake na Himdi. Amesifika kwa uwezo na nguvu kamili, na kwa utekelezaji wa utashi Wake na Ana Sifa ya kuwa na Hikmah kamili na yenye kukizunguka kila kitu.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
فَأَمَّا الَّذِينَ شَقُوا فَفِي النَّارِ لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَشَهِيقٌ﴿١٠٦﴾
Basi ama wale walio mashakani, basi watakuwa motoni, lao humo ni upumuaji pumzi kwa mngurumo na uvutaji pumzi kwa mkoromo.
خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ﴿١٠٧﴾
Ni wenye kudumu humo zitakavyodumu mbingu na ardhi isipokuwa Atakavyo Rabb wako. Hakika Rabb wako Anafanya Atakavyo.
وَأَمَّا الَّذِينَ سُعِدُوا فَفِي الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۖ عَطَاءً غَيْرَ مَجْذُوذٍ﴿١٠٨﴾
Na ama wale walio furahani, basi watakuwa katika Jannah, ni wenye kudumu humo zitakavyodumu mbingu na ardhi isipokuwa Atakavyo Rabb wako. Ni hiba isiyokatizwa. [Hud (11): 106-108]