56-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ummah Wake Utashudhuia Umati Zote Za Nyuma
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
56-Ummah Wake Utashudhuia Umati Zote Za Nyuma
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ
Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu. [Al-Baqarah: 143]
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " يَجِيءُ نُوحٌ وَأُمَّتُهُ فَيَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى هَلْ بَلَّغْتَ فَيَقُولُ نَعَمْ، أَىْ رَبِّ. فَيَقُولُ لأُمَّتِهِ هَلْ بَلَّغَكُمْ فَيَقُولُونَ لاَ، مَا جَاءَنَا مِنْ نَبِيٍّ. فَيَقُولُ لِنُوحٍ مَنْ يَشْهَدُ لَكَ فَيَقُولُ مُحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم وَأُمَّتُهُ، فَنَشْهَدُ أَنَّهُ قَدْ بَلَّغَ، وَهْوَ قَوْلُهُ جَلَّ ذِكْرُهُ (( وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ)) وَالْوَسَطُ الْعَدْلُ ". البخاري
Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ataitwa Nuwh Siku ya Qiyaamah ataulizwa: Je, umebalighisha ujumbe? Atasema: Naam. Wataitwa watu wake wataulizwa: Je, alikufikishieni ujumbe? Watasema: Hakutujia mwonyaji wala hakuna aliyetumwa kwetu. Ataulizwa Nuwh: Nani mwenye kukushuhudia hayo? Atasema: Muhammad na Ummah wake. Akasema: Hiyo ndio maana kauli Yake:
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ
Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu. Akasema: “Waswatwaa, maana yake ni uadilifu basi mtatoa ushahidi (kuhusu Nuwh) kubalighisha ujumbe na kisha nitakuwa shahidi wenu.” [Ahmad (3/32) na Al-Bukhaariy pia kama hivyo (4487)]
Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَجَاهِدُوا فِي اللَّـهِ حَقَّ جِهَادِهِ ۚ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ۚ مِّلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ ۚ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِن قَبْلُ وَفِي هَـٰذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ ۚ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَاعْتَصِمُوا بِاللَّـهِ هُوَ مَوْلَاكُمْ ۖ فَنِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ ﴿٧٨﴾
Na fanyeni jihaad katika njia ya Allaah kama inavyostahiki kufanyiwa jihaad. Yeye Ndiye Amekuteueni na Hakukufanyieni ugumu wowote ule katika Dini. Mila ya baba yenu Ibraahiym. Yeye (Allaah) Ndiye Aliyekuiteni Waislamu hapo zamani na pia katika hii (Qur-aan). Ili Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) awe shahidi juu yenu, nanyi muwe mashahidi juu ya watu. [Al-Hajj: 78]
Imaam As-Sa’diy amesema kuhusu kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ
nanyi muwe mashahidi juu ya watu.
Kwa sababu ya kuwa kwenu nyinyi Waislamu ni Ummah bora kabisa uliotolewa kwa watu, Ummah wa wastani kwa uadilifu, basi mtashahudia Rusuli wote kwamba wamebalighisha ujumbe kwa Ummah zao, na mtashuhudia kwa Ummah zote kwamba Rusuli wao wamebalighisha ujumbe kutokana na yale ambayo Allaah Amekujulisheni katika Kitabu Chake (Qur-aan). [Tafsiyr As’Sa’diy]
Ummah wa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ni Ummah bora kabisa ni kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾
Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Ahlul-Kitaabi ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wanaoamini na wengi wao ni mafasiki [Aal-‘Imraan:110]