57-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Dini Yake Ndio Itakayoshinda Dini Zote
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
57-Dini Yake Ndio Itakayoshinda Dini Zote
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا﴿٢٨﴾
Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote. Na Allaah Anatosha kuwa ni Shahidi. [Al-Fat-h:28]
Qiyaamah hakitasimama hadi Dini ya Kiislaam ishinde Dini zote, na hii imeshaanza kudhihirika ulimwenguni kutokana na matukio kadhaa yaliyosababisha watu wengi kuingia katika Uislaam.
Na katika Dalili kumi kubwa za kusimama Qiyaamah zipo Hadiyth kadhaa zinazoelezea hayo mojawapo ifuatayo:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَة قَالَ : قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((يَنْزِل عِيسَى اِبْن مَرْيَم فَيَقْتُل الْخِنْزِير وَيَمْحُو الصَّلِيب وَتُجْمَع لَهُ الصَّلَاة وَيُعْطِي الْمَال حَتَّى لَا يُقْبَل وَيَضَع الْخَرَاج وَيَنْزِل الرَّوْحَاء فَيَحُجّ مِنْهَا أَوْ يَعْتَمِر أَوْ يَجْمَعهُمَا)) أحمد
Kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((‘Iysaa mwana wa Maryam atateremka na kuua nguruwe, atavunja misalaba, ataimamisha watu katika Swalaah ya Jamaa, na kutoa mali hadi hakuna atakayetaka kupokea tena. Ataondosha jizya (kodi) na atakwenda Ar-Rawhaa ambako ataelekea kutekeleza Hajj, ‘Umrah au zote mbili)) [Ahmad]
Imaam Atw-Twabariy amesema kuhusu kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ ۚ
Ili Aishindishe juu ya dini zote.
“Hivyo ni kubatilisha millah (dini) zote hadi kwamba hakutakuwa na Dini nyingine isipokuwa hiyo, na hivyo ndivyo ilivyokuwa mpaka ‘Iysaa mwana wa Maryam ashuke na kumuua Ad-Dajaal, hapo Dini zote zitabatilishwa isipokuwa Dini ya Allaah aliyomtuma nayo Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na Uislaam ushinde juu ya dini zote."
Na Hadiyth nyenginezo zifuatazo:
عَنْ تَمِيمٍ الدَّارِيِّ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَيَبْلُغَنَّ هَذَا الْأَمْرُ مَا بَلَغَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَلَا يَتْرُكُ اللَّهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ هَذَا الدِّينَ بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ بِذُلِّ ذَلِيلٍ عِزًّا يُعِزُّ اللَّهُ بِهِ الْإِسْلَامَ وَذُلًّا يُذِلُّ اللَّهُ بِهِ الْكُفْرَ
Tamiym Ad-Daariyy amesimulia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jambo hili (Uislaam) hakika litafika kila mahali palipoguswa na usiku na mchana. Allaah Hatoacha nyumba au makazi isipokuwa Allaah Ataingizi Dini hii kwa ‘izza (utukufu) ambao watukufu watajaaliwa taadhima na wadhalili watadhalilika. Allaah Atawapa utukufu watukufu kwa Uislaam na Atawadhalilisha wadhalili kwa Ukafiri. [Ahmad]
Na pia,
عَن الْمِقْدَاد بن الْأسود قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: " يَقُولُ لَا يَبْقَى عَلَى ظَهْرِ الْأَرْضِ بَيْتُ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ كلمة الاسلام بعز عَزِيز أَو ذل ذليل إِمَّا يعزهم الله عز وَجل فَيَجْعَلُهُمْ مِنْ أَهْلِهَا أَوْ يُذِلُّهُمْ فَيَدِينُونَ لَهَا رَوَاهُ أَحْمد
Miqdaad bin Al-Aswad amesimulia: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Haitasalia juu ya ardhi (duniani) nyumba ya udongo wala hema la nywele za ngamia isipokuwa Allaah Ataingiza humo neno la Islaam kwa ‘izza (utukufu) ambao watukufu watajaaliwa taadhima na wadhalili watadhalilika ima Allaah (‘Azza wa Jalla) Awape utukufu wakazi na kuwajaalia wawe katika watu Wake, au Awadhalilishe na wawe duni mbele Yake.” [Ahmad, Swahiyh Ibn Maajah (6701)]
Na Kauli Zake nyenginezo Allaah (سبحانه وتعالى):
هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٩﴾
Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina. [Asw-Swaff: 9]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٣٣﴾
Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina. [At-Tawbah: 33]