032-Asbaabun-Nuzuwl: As-Sajdah Aayah 16: تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
032-Asbaabun-Nuzuwl: As-Sajdah Aayah 16
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿١٦﴾ فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٧﴾
Mbavu zao zinatengana na vitanda, wanamuomba Rabb wao kwa khofu na matumaini, na katika yale Tuliyowaruzuku wanatoa. Basi nafsi yoyote haijui yaliyofichiwa katika yanayoburudisha macho. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [As-Sajdah (32:16)]
Sababun-Nuzuwl:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي زِيَادٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الأُوَيْسِيُّ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ بِلاَلٍ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّ هَذِهِ الآيَةَ : ((تتَجَافَى، جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ)) نَزَلَتْ فِي انْتِظَارِ هَذِهِ الصَّلاَةِ الَّتِي تُدْعَى الْعَتَمَةَ . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ غَرِيبٌ لاَ نَعْرِفُهُ إِلاَّ مِنْ هَذَا الْوَجْهِ
Ametuhadithia ‘Abdullaah bin Abiy Ziyaad, ametuhadithia ‘Abdul-‘Aziyz bin ‘Abdillaah Al-Uwaysiy toka kwa Sulaymaan bin Bilaal toka kwa Yahyaa bin Sa’iyd toka kwa Anas bin Maalik kuhusiana na Aayaah hii:
تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ
Mbavu zao zinatengana na vitanda
Ni kuwa iliteremka kuzungumzia kuisubiri Swalaah iitwayo Al-‘Atamah. [At-Tirmidhiy katika Mujallad wa Nne ukurasa wa 161. Hii ni Hadiyth Hasan Swahiyh, hatuijui ila kwa picha hii. Ibn Jariyr ameikhariji katika Mujallad wa Kumi na Mbili ukurasa wa 100. Na Al-Haafidh Ibn Kathiyr amesema katika Tafsiyr yake kuwa Sanad yake ni Jayyid].