108-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Kawthar: إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ

 

 

 

Sababu Za Kuteremshwa

(Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Suwrah Al-Kawthar

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

108:Al-Kawthar:  

 

 

إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ ﴿١﴾

1. Hakika Sisi Tumekupa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Al-Kawthar (Mto katika Jannah).

 

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾

2. Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja kwa ajili Yake.

 

إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الْأَبْتَرُ ﴿٣﴾

3. Hakika mbaya wako, yeye ndiye atakayekatiliwa mbali (kizazi na kila khayr).

 

 

عن عكرمة عن ابن عباس قال: قدم كعب بن الأشرف مكة فقالت له قريش: أنت سيدهم ألا ترى إلى هذا الصنبور المنبتر من قومه يزعم أنه خير منا ونحن أهل الحجيج وأهل السدانة وأهل السقاية، فقال: أنتم خير منه، قال: فنزلت ((إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الْأَبْتَرُ))

 

Kutoka kwa ‘Ikrimah kutoka kwa Ibn ‘Abbass amesema: Ka’b bin Ashraf alifika Makkah na Quraysh wakamwambia: “Wewe ni bwana wao je, huoni kuwa Swanbuwr hii iliyokatika kizazi chake kutoka kwa watu wake anadai kuwa yeye ni bora kuliko sisi na sisi ndio watu wenye kushughulikia mahujaji na watu wa As-Sadaanah na watu wa Siqaayah?” Akasema Ka’b: “Ninyi ni bora kuliko yeye”. Akasema: Ikateremka: “Hakika mbaya wako, yeye ndiye atakayekatiliwa mbali (kizazi na kila khayr)” [Imepokewa na Al-Bazaar kwa Isnaad Swahiyh]

 

Hadityh hii imepokewa na Ibn Jurayj (3/330) kutoka katika njia ya Shaykh wake Muhammad bin Bashaar amehadithia Ibn Abi ‘Adiyy kutoka kwake. Na akazidisha ndani yake imeteremka juu yake: “Je, huoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanakhiari upotofu na wanataka mpotee njia?...” [An-Nisaa 4: 44] mpaka kauli Yake: “Mwenye kunusuru”

 

 

Pia,

عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: بَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَوْمٍ بَيْنَ أَظْهُرِنَا إِذْ أَغْفَى إِغْفَاءَةً ثُمَّ رَفَعَ رَأْسَهُ مُتَبَسِّمًا فَقُلْنَا: مَا أَضْحَكَكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟  قَالَ: ((أُنْزِلَتْ عَلَىَّ آنِفًا سُورَةٌ ))‏. فَقَرَأَ: (( بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ)).‏ ثُمَّ قَالَ: ((أَتَدْرُونَ مَا الْكَوْثَرُ؟)). فَقُلْنَا اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ.‏ قَالَ: ((فَإِنَّهُ نَهْرٌ وَعَدَنِيهِ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ عَلَيْهِ خَيْرٌ كَثِيرٌ هُوَ حَوْضٌ تَرِدُ عَلَيْهِ أُمَّتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ آنِيَتُهُ عَدَدُ النُّجُومِ فَيُخْتَلَجُ الْعَبْدُ مِنْهُمْ فَأَقُولُ رَبِّ إِنَّهُ مِنْ أُمَّتِي‏.‏ فَيَقُولُ مَا تَدْرِي مَا أَحْدَثَتْ بَعْدَكَ))‏.‏ زَادَ ابْنُ حُجْرٍ فِي حَدِيثِهِ بَيْنَ أَظْهُرِنَا فِي الْمَسْجِدِ‏.‏ وَقَالَ:‏ ((مَا أَحْدَثَ بَعْدَكَ))‏.

 

Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa pamoja nasi akawa amepitiwa na lepe la usingizi kisha akanyanyua kichwa chake juu huku akitabasamu, tukasema: Ni kitu gani kimekufurahisha ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Imeniteremkia sasa hivi Suwrah: (Akaisoma Suwrah Al-Kawthar).

 

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ *

Hakika Sisi Tumekupa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Al-Kawthar (Mto katika Jannah). Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja.  Hakika mbaya wako, yeye ndiye atakayekatiliwa mbali (kizazi na kila kheri).”  [Al-Kawthar: (108)]  

 

Kisha akasema: “Je, mnajua ni nini Al-Kawthar?” Tukajibu: Allaah na Rasuli Wake Ndio Wajuao zaidi. Akasema: “Huo ni mto ambao Allaah (عزّ وجلّ) Ameniahidi. Una kheri nyingi sana, nao una hodhi lake ambalo Ummah wangu watakusudia kulifikia Siku ya Qiyaamah. Vyombo vyake (au bilauri) ni idadi ya nyota. Mja miongoni mwao atatolewa mbali atengwe. Nitasema: Ee Rabb! Hakika yeye ni katika Ummah wangu!  Allaah Atasema: Hujui nini alizusha baada yako!”

 

Ibn Hujri amezidisha katika Hadiyth yake: Alikuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amekaa kitako pamoja nasi Msikitini. Na (Allaah) Atasema: “Hujui walichokizusha baada yako!” [Muslim – Kitaab Asw-Swalaah - Mlango wa hoja anayesema kuwa Al-Basmalah ni Aayah katika kila mwanzo wa Suwrah isipokuwa Suwrah Al-Baraa (At-Tawbah)] 

 

 

Pia,

 

بينما ذاتَ يومٍ بينَ أظهرِنا يريدُ النَّبيَّ صلَّى اللَّهُ عليهِ وسلَّمَ إذ أغفى إغفاءةً ثمَّ رفعَ رأسهُ متبسِّمًا فقلنا لهُ: ما أضحكَكَ يا رسولَ اللَّهِ؟  قالَ: نزلت عليَّ آنفًا سورةٌ: ((بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ)) ثمَّ قالَ: ((هل تدرونَ ما الكوثرُ؟)) قلنا اللَّهُ ورسولُهُ أعلم قالَ: ((فإنَّهُ نهرٌ وعدنيهِ ربِّي في الجنَّةِ آنيتُهُ أكثرُ من عددِ الكواكبِ ترِدُهُ عليَّ أمَّتي فيختلِجُ العبدُ منهم فأقولُ يا ربِّ إنَّهُ من أمَّتي فيقولُ لي إنَّكَ لا تدري ما أحدثَ بعدَكَظ)).

Siku moja tulikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  na akapitiwa na usingizi mara akanyanyua kichwa chake huku akitabasamu. Tukamuuliza ni nini kinachokuchekesha ee Rasuli wa Allaah?” Akajibu: “Hivi imeniteremkia: 

 

((بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ))

 

[Al-Kawthar: 108].

 

Kisha akauliza, Je, mnajua nini Al-Kawthar? Tukasema Allaah na Rasuli Wake ndio wanaojua.” Akasema: “Ni mto wa wa Jannah ambao Allaah Ameniahidi, na vyombo vyake (au bilauri) ni idadi ya nyota. Na  Ummah wangu watanifikia (katika hodhi) lakini  mtu atotelewa hapo na kutengwa, kisha nitasema, Ee Rabb wangu huyo ni katika Ummah wangu! Na hapo Ataniambi: Hakika wewe hujui alichokizua baada yako.” [Mpokeaji ni Anas bin Maalik, katika Swahiyh An-Nasaaiy cha Imaam Al-Albaaniy (uk. 903) hitimisho la hukumu ya mwenye kuzua. Angalia Swahiyh sharh ya Hadiyth namba (21618)]

 

Pia,

 

Amepokea Muslim, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy kutoka kwa Anas [Muslim: (1/300), Abuu Daawuwd: (5/110) na An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (6/533) na tamko ni la Muslim amesema: “Wakati Rasuli wa Allaah yuko mbele yetu Msikitini, ghafla alisinzia usinziaji wa mara moja kisha akanyanyua kichwa chake hali ya kuwa anatabasamu tukasema: Ni jambo gani ambalo linakuchekesha ee Rasuli wa Allaah?” Akasema: “Kwa hakika imeteremshwa kwangu punde Suwrah….” (akasoma Suwrah ya Al-Kawthar).

 

 

Share