066-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tahriym Aayah 4-5: إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
At-Tahriym Aayah 4-5
Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا ۖ وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ﴿٤﴾
4. Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allaah (ni kheri kwenu) kwani kwa hakika nyoyo zenu zimeelemea (yanayomchukiza Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم). Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allaah Ndiye Mlinzi Msaidizi wake na Jibriyl na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia.
عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ ثَيِّبَاتٍ وَأَبْكَارًا﴿٥﴾
5. Akikutalikini, asaa Rabb Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi; Waislamu, Waumini, watiifu na wanyenyekevu, wanaotubia, wenye kufanya ‘ibaadah, wanaofunga Swiyaam au wanaohajiri kwa ajili ya Allaah, wajane, na walio bikra.
Sababun-Nuzuwl:
عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه ، قَالَ لَمَّا اعْتَزَلَ نَبِيُّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم نِسَاءَهُ قَالَ: دَخَلْتُ الْمَسْجِدَ فَإِذَا النَّاسُ يَنْكُتُونَ بِالْحَصَى وَيَقُولُونَ: طَلَّقَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم نِسَاءَهُ وَذَلِكَ قَبْلَ أَنْ يُؤْمَرْنَ بِالْحِجَابِ فَقَالَ عُمَرُ: فَقُلْتُ لأَعْلَمَنَّ ذَلِكَ الْيَوْمَ قَالَ فَدَخَلْتُ عَلَى عَائِشَةَ فَقُلْتُ: يَا بِنْتَ أَبِي بَكْرٍ أَقَدْ بَلَغَ مِنْ شَأْنِكِ أَنْ تُؤْذِي رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم؟ فَقَالَتْ: مَا لِي وَمَا لَكَ يَا ابْنَ الْخَطَّابِ عَلَيْكَ بِعَيْبَتِكَ . قَالَ: فَدَخَلْتُ عَلَى حَفْصَةَ بِنْتِ عُمَرَ فَقُلْتُ لَهَا: يَا حَفْصَةُ أَقَدْ بَلَغَ مِنْ شَأْنِكِ أَنْ تُؤْذِي رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَاللَّهِ لَقَدْ عَلِمْتِ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لاَ يُحِبُّكِ وَلَوْلاَ أَنَا لَطَلَّقَكِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم . فَبَكَتْ أَشَدَّ الْبُكَاءِ فَقُلْتُ لَهَا: أَيْنَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم؟ قَالَتْ: هُوَ فِي خِزَانَتِهِ فِي الْمَشْرُبَةِ . فَدَخَلْتُ فَإِذَا أَنَا بِرَبَاحٍ غُلاَمِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَاعِدًا عَلَى أُسْكُفَّةِ الْمَشْرُبَةِ مُدَلٍّ رِجْلَيْهِ عَلَى نَقِيرٍ مِنْ خَشَبٍ وَهُوَ جِذْعٌ يَرْقَى عَلَيْهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَيَنْحَدِرُ فَنَادَيْتُ: يَا رَبَاحُ اسْتَأْذِنْ لِي عِنْدَكَ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم . فَنَظَرَ رَبَاحٌ إِلَى الْغُرْفَةِ ثُمَّ نَظَرَ إِلَىَّ فَلَمْ يَقُلْ شَيْئًا ثُمَّ قُلْتُ: يَا رَبَاحُ اسْتَأْذِنْ لِي عِنْدَكَ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم . فَنَظَرَ رَبَاحٌ إِلَى الْغُرْفَةِ ثُمَّ نَظَرَ إِلَىَّ فَلَمْ يَقُلْ شَيْئًا ثُمَّ رَفَعْتُ صَوْتِي فَقُلْتُ: يَا رَبَاحُ اسْتَأْذِنْ لِي عِنْدَكَ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَإِنِّي أَظُنُّ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ظَنَّ أَنِّي جِئْتُ مِنْ أَجْلِ حَفْصَةَ وَاللَّهِ لَئِنْ أَمَرَنِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِضَرْبِ عُنُقِهَا لأَضْرِبَنَّ عُنُقَهَا . وَرَفَعْتُ صَوْتِي فَأَوْمَأَ إِلَىَّ أَنِ ارْقَهْ فَدَخَلْتُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ مُضْطَجِعٌ عَلَى حَصِيرٍ فَجَلَسْتُ فَأَدْنَى عَلَيْهِ إِزَارَهُ وَلَيْسَ عَلَيْهِ غَيْرُهُ وَإِذَا الْحَصِيرُ قَدْ أَثَّرَ فِي جَنْبِهِ فَنَظَرْتُ بِبَصَرِي فِي خِزَانَةِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَإِذَا أَنَا بِقَبْضَةٍ مِنْ شَعِيرٍ نَحْوِ الصَّاعِ وَمِثْلِهَا قَرَظًا فِي نَاحِيَةِ الْغُرْفَةِ وَإِذَا أَفِيقٌ مُعَلَّقٌ – قَالَ: فَابْتَدَرَتْ عَيْنَاىَ قَالَ: ((مَا يُبْكِيكَ يَا ابْنَ الْخَطَّابِ)) . قُلْتُ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ وَمَا لِي لاَ أَبْكِي وَهَذَا الْحَصِيرُ قَدْ أَثَّرَ فِي جَنْبِكَ وَهَذِهِ خِزَانَتُكَ لاَ أَرَى فِيهَا إِلاَّ مَا أَرَى وَذَاكَ قَيْصَرُ وَكِسْرَى فِي الثِّمَارِ وَالأَنْهَارِ وَأَنْتَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَصَفْوَتُهُ وَهَذِهِ خِزَانَتُكَ . فَقَالَ: ((يَا ابْنَ الْخَطَّابِ أَلاَ تَرْضَى أَنْ تَكُونَ لَنَا الآخِرَةُ وَلَهُمُ الدُّنْيَا)) . قُلْتُ: بَلَى - قَالَ : وَدَخَلْتُ عَلَيْهِ حِينَ دَخَلْتُ وَأَنَا أَرَى فِي وَجْهِهِ الْغَضَبَ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ مَا يَشُقُّ عَلَيْكَ مِنْ شَأْنِ النِّسَاءِ فَإِنْ كُنْتَ طَلَّقْتَهُنَّ فَإِنَّ اللَّهَ مَعَكَ وَمَلاَئِكَتَهُ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَأَنَا وَأَبُو بَكْرٍ وَالْمُؤْمِنُونَ مَعَكَ وَقَلَّمَا تَكَلَّمْتُ وَأَحْمَدُ اللَّهَ بِكَلاَمٍ إِلاَّ رَجَوْتُ أَنْ يَكُونَ اللَّهُ يُصَدِّقُ قَوْلِي الَّذِي أَقُولُ وَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ آيَةُ التَّخْيِيرِ: ((عَسَى رَبُّهُ إِنْ طَلَّقَكُنَّ أَنْ يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِنْكُنَّ...)) ))وَإِنْ تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّهَ هُوَ مَوْلاَهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمَلاَئِكَةُ بَعْدَ ذَلِكَ ظَهِيرٌ(( وَكَانَتْ عَائِشَةُ بِنْتُ أَبِي بَكْرٍ وَحَفْصَةُ تَظَاهَرَانِ عَلَى سَائِرِ نِسَاءِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَطَلَّقْتَهُنَّ؟ قَالَ: ((لاَ)) قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنِّي دَخَلْتُ الْمَسْجِدَ وَالْمُسْلِمُونَ يَنْكُتُونَ بِالْحَصَى يَقُولُونَ طَلَّقَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم نِسَاءَهُ أَفَأَنْزِلُ فَأُخْبِرَهُمْ أَنَّكَ لَمْ تُطَلِّقْهُنَّ؟ قَالَ: ((نَعَمْ إِنْ شِئْتَ)) فَلَمْ أَزَلْ أُحَدِّثُهُ حَتَّى تَحَسَّرَ الْغَضَبُ عَنْ وَجْهِهِ وَحَتَّى كَشَرَ فَضَحِكَ وَكَانَ مِنْ أَحْسَنِ النَّاسِ ثَغْرًا ثُمَّ نَزَلَ نَبِيُّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَنَزَلْتُ فَنَزَلْتُ أَتَشَبَّثُ بِالْجِذْعِ وَنَزَلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَأَنَّمَا يَمْشِي عَلَى الأَرْضِ مَا يَمَسُّهُ بِيَدِهِ فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّمَا كُنْتَ فِي الْغُرْفَةِ تِسْعَةً وَعِشْرِينَ . قَالَ: ((إِنَّ الشَّهْرَ يَكُونُ تِسْعًا وَعِشْرِينَ)) فقُمْتُ عَلَى بَابِ الْمَسْجِدِ فَنَادَيْتُ بِأَعْلَى صَوْتِي لَمْ يُطَلِّقْ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم نِسَاءَهُ . وَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ : ((وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِنَ الأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَى أُولِي الأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنْبِطُونَهُ مِنْهُمْ)) فَكُنْتُ أَنَا اسْتَنْبَطْتُ ذَلِكَ الأَمْرَ وَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ آيَةَ التَّخْيِيرِ .
Kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khatwaab (رضي الله عنه) amesema: Pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipojitenga na wake zake, niliingia Msikitini nikaona watu wanapiga ardhi kwa vijiwe huku wakisema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amewataliki wake zake.” Hivyo ilikuwa kabla ya kuamrishwa kwao hijaab. Nikasema ndani ya nafsi yangu: “Nitalijua hilo leo.” Akasema: Akaingia kwa ‘Aaishah akasema: “Ee binti wa Abuu Bakr hivi umefikia kumuudhi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?” ‘Aaishah akasema: “Una nini ee Ibn Al-Khatwaab shughulika na ya kwako.” (Yaani kampe mawaidha haya mwanao Hafswa). Akasema: “Nikaingia kwa Hafswah nikamwambia: “Ee Hafswah, hivi umefikia kumuudhi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na ilhali umeshajua kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakupendi na lau si mimi basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) angelikutaliki.” Hafswah akalia kilio kikubwa (cha uchungu) nikamuuliza: “Yuko wapi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?” Akasema: “Yupo darini.” Nikaingia nikamkuta Rabaah ghulamu wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa amekaa katika ukingo wa dirisha akining’iniza mguu wake katika kipande cha mbao cha gogo la mtende ambacho huwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akilitumia na kupandia (kuingia chumbanii mwake) na kuteremkia. Nikaita: “Ee Rabaah! Niombee ruhusa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).” Rabaah akaangalia chumbani kisha akaniangalia mimi na hakusema kitu. Kisha nikamuita tena nikasema: “Ee Rabaah niombee ruhusa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).” Rabaah akaangalia chumbani kisha akaniangalia mimi na hakusema chochote. Kisha nikanyanyua sauti yangu na kusema: “Ee Rabaah niombee ruhusa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa hakika mimi nadhani kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) anajua kuwa nimekuja kuhusiana na Hafaswah, Wa-Allaahi pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiniamrisha niikate shingo yake (nimuue), basi hakika mimi nitaikata!” Nikapandisha sauti yangu akaniashiria nipande, nikaingia kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) (nikamkuta) akiwa amelala kwa ubavu juu ya mkeka. Nikakaa, na (Rabaah) akamsogezea izari yake, na hana nyingine zaidi ya hiyo. Nikagutuka kuona alama za mkeka zimechora kwenye ubavu wake. Halafu nikapembua kwa jicho langu kwenye stoo ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na nikastuka kuona shayiri kiasi cha pishi moja ya kujaa kiganja cha mkono na kiasi kama hicho hicho cha gundi upande wa chumba ambako kuna ngozi mbichi imetundikwa (upande mmoja). Hapo hapo macho yangu yakatiririka machozi. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Kinakuliza nini ee Ibn Al-Khattwaab?)) Nikasema: “Ee Nabiy wa Allaah, kwanini nisilie ilhali huu mkeka umekufanyia alama mwilini mwako na khazana (stoo) yako sioni kilichomo ila kile ninachokiona na ilhali kule kuna (Wafalme) Qayswar (Ceaser) na Kisraa wana matunda na mito (wanaishi kifakhari), basi vipi iwe wewe Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye Allaah Amekuchagua (huna lolote) hii ndio khazana yako?” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Ee Ibn Al-Khattwaab je huridhii sisi tukawa na Aakhirah na wao wakawa na dunia?)). Nikasema: “Naam!” (nakubaliana nawe). Nilipoingia kwake nikaona ghadhabu usoni mwake. Nikasema: “Ee Rasuli wa Allaah je, umepata matatizo gani na wake zako? Ikiwa umewataliki basi Allaah Yu pamoja nawe na Malaika na Jibriyl na Mikaaiyl na mimi na Abuu Bakr na Waumini tu pamoja nawe.” Na mara chache nilipozungumza na kumshukuru Allaah kwa maneno yangu, basi hutarajia Allaah Asadikishe kauli yangu ninayosema, Ikateremka Aayah hii Aayah ya At-Takh-yiyr (chaguo):
عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ
Akikutalikini, asaa Rabb Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi;
وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ
Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allaah Ndiye Mlinzi Msaidizi wake na Jibriyl na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia.
Na ilikuwa ni ‘Aaishah bint wa Abuu Bakr na Hafswah ndio walioshikilia kuliko wake wengineo wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) (kumtia dhiki katika kuomba mali). Nikasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Je umewataliki?” Akasema: ((Hapana!)). Nikasema: “Ee Rasuli wa Allaah, mimi niliingia Msikitini na Waislamu wanafanya mchezo wa kurushiana vijiwe (wakiwa mawazoni) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amewataliki wake zake. Je niende kuwajulisha kuwa hukuwataliki?” Akasema: ((Naam ukipenda)). Basi nikaendelea kuongea naye mpaka ghadhabu ikapotea usoni mwake na uso wake ukawa na utulivu wa maumbile yake, akacheka na meno yake yakaonekana naye alikuwa na mwanya mzuri zaidi kuliko watu wengineo. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akateremka, nami nikateremka huku nikikamata gogo la mtende na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiteremka chini (kwa wepesi kabisa) kama vile anavyotembea ardhini bila ya kukamata chochote (cha sapoti). Nikasema: “Ee Rasuli wa Allaah. Ulibakia chumbani kwako siku ishirini na tisa.” Akasema: ((Miezi (hutokea kuwa) ni siku ishiri na tisa.) Nikasimama mlangoni mwa Msikiti nikanadi kwa sauti ya juu kabisa: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuwataliki wake zake!” Hapo ikateremka:
وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ ۗ
Na linapowafikia jambo lolote la amani au la khofu hulitangaza. Na lau wangelirudisha kwa Rasuli na kwa wenye madaraka kati yao, wangelijua wale wanaotafiti wakabainisha ya sahihi miongoni mwao. [An-Nisaa: 83]
Ikawa ni mimi niliyeifahamu kwa kina amri hiyo na Allaah (عزّ وجلّ) Akateremsha Aayah ya At-Takh-yiyr.”
[Muslim Kitaab Atw-Twalaaq]
Riwaayah nyenginezo za Asbaab Nuzuwl katika Hadiyth zifuatazo:
عن عمر ابن الخطاب رضي الله عنه قال: اجْتَمَعَ نِسَاءُ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي الْغَيْرَةِ عَلَيْهِ فَقُلْتُ لَهُنَّ عَسَى رَبُّهُ إِنْ طَلَّقَكُنَّ أَنْ يُبَدِّلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِنْكُنَّ. فَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ.
Kutoka kwa ‘Umar (رضي الله عنه) kwamba Wake wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) walikujumuika kuwa na wivu naye, nikawaambia: “Akikutalikini, asaa Rabb Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi.” Ikateremka Aayah hii:
عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ ثَيِّبَاتٍ وَأَبْكَارًا﴿٥﴾
5. Akikutalikini, asaa Rabb Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi; Waislamu, Waumini, watiifu na wanyenyekevu, wanaotubia, wenye kufanya ‘ibaadah, wanaofunga Swiyaam au wanaohajiri kwa ajili ya Allaah, wajane, na walio bikra.
[Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]
Pia:
عَنْ أَنَسٍ، قَالَ قَالَ عُمَرُ وَافَقْتُ اللَّهَ فِي ثَلاَثٍ أَوْ وَافَقَنِي رَبِّي فِي ثَلاَثٍ ـ قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، لَوِ اتَّخَذْتَ مَقَامَ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى وَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ يَدْخُلُ عَلَيْكَ الْبَرُّ وَالْفَاجِرُ، فَلَوْ أَمَرْتَ أُمَّهَاتِ الْمُؤْمِنِينَ بِالْحِجَابِ فَأَنْزَلَ اللَّهُ آيَةَ الْحِجَابِ قَالَ وَبَلَغَنِي مُعَاتَبَةُ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم بَعْضَ نِسَائِهِ، فَدَخَلْتُ عَلَيْهِنَّ قُلْتُ إِنِ انْتَهَيْتُنَّ أَوْ لَيُبَدِّلَنَّ اللَّهُ رَسُولَهُ صلى الله عليه وسلم خَيْرًا مِنْكُنَّ. حَتَّى أَتَيْتُ إِحْدَى نِسَائِهِ، قَالَتْ يَا عُمَرُ، أَمَا فِي رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مَا يَعِظُ نِسَاءَهُ حَتَّى تَعِظَهُنَّ أَنْتَ فَأَنْزَلَ اللَّهُ: ((عَسَى رَبُّهُ إِنْ طَلَّقَكُنَّ أَنْ يُبَدِّلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِنْكُنَّ مُسْلِمَاتٍ)) الآيَةَ.
Anas amehadithia kwamba ‘Umar Ibn Al-Khatwaab amesema: “Allaah Ameniwafikia kuhusu mambo matatu.” Au “Rabb wangu Amewafikiana nami kuhusu mambo matatu: Nilisema: “Ee Rasuli wa Allaah, ungelifanya mahali aliposimama Ibraahiym kuwa ni mahali pa kuswalia.” Ikateremka:
وَاتَّخِذُوا مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى ۖ
Na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia. [Al-Baqarah: 125]
Na kuhusu Aayah ya Hijaab nilisema: “Ee Rasuli wa Allaah, ungeliwaamrisha wake zako wajiwekee hijaab kwani wao wanaongea na wema na waovu.” Ikateremka Aayah ya hijaab (Al-Ahzaab: 53). Wakajumuika wake wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa na wivu naye, nikawaambia: “Akikutalikini, asaa Rabb Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi.” Ikateremka Aayah hii:
عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ ثَيِّبَاتٍ وَأَبْكَارًا﴿٥﴾
5. Akikutalikini, asaa Rabb Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi; Waislamu, Waumini, watiifu na wanyenyekevu, wanaotubia, wenye kufanya ‘ibaadah, wanaofunga Swiyaam au wanaohajiri kwa ajili ya Allaah, wajane, na walio bikra.
[Al-Bukhaariy Kitaab Asw-Swalaah)
Pia:
عن عمر ابن الخطاب رضي الله عنه قال: وَافَقْتُ اللَّهَ فِي ثَلاَثٍ ـ أَوْ وَافَقَنِي رَبِّي فِي ثَلاَثٍ ـ قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، لَوِ اتَّخَذْتَ مَقَامَ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى وَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ يَدْخُلُ عَلَيْكَ الْبَرُّ وَالْفَاجِرُ، فَلَوْ أَمَرْتَ أُمَّهَاتِ الْمُؤْمِنِينَ بِالْحِجَابِ فَأَنْزَلَ اللَّهُ آيَةَ الْحِجَابِ قَالَ وَبَلَغَنِي مُعَاتَبَةُ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم بَعْضَ نِسَائِهِ، فَدَخَلْتُ عَلَيْهِنَّ قُلْتُ إِنِ انْتَهَيْتُنَّ أَوْ لَيُبَدِّلَنَّ اللَّهُ رَسُولَهُ صلى الله عليه وسلم خَيْرًا مِنْكُنَّ. حَتَّى أَتَيْتُ إِحْدَى نِسَائِهِ، قَالَتْ يَا عُمَرُ، أَمَا فِي رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مَا يَعِظُ نِسَاءَهُ حَتَّى تَعِظَهُنَّ أَنْتَ فَأَنْزَلَ اللَّهُ: ((عَسَى رَبُّهُ إِنْ طَلَّقَكُنَّ أَنْ يُبَدِّلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِنْكُنَّ مُسْلِمَاتٍ...)) الآيَةَ.
Kutoka kwa Anas kwamba ‘Umar Ibn Al-Khatwaab amesema: ”Allaah Ameniwafikia kuhusu mambo matatu.” Au “Rabb wangu Amewafikiana nami kuhusu mambo matatu: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah, ungelifanya mahali aliposimama Ibraahiym kuwa ni mahali pa kuswali. Na nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, wanaingia kwako wema na waovu basi lau ungeliwaamrisha hijaab Mama wa Waumini. Ikateremka Aayah ya hijaab. [Al-Ahzaab: 53]. Ikanifikia habari kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amewakemea baadhi ya wake zake. Nikawaendea nikasema: Ima mkome (kumuudhi Nabiy) au Allaah Atambadilishia Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) (wake) walio bora kulikoni nyinyi. Nilipomfikia mmoja wa mke wake alisema: Ee ‘Umar jambo gani ambalo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuwaidhi wake zake hata wewe ndiye utuwaidi? Ikateremka:
عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ ثَيِّبَاتٍ وَأَبْكَارًا﴿٥﴾
5. Akikutalikini, asaa Rabb Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi; Waislamu, Waumini, watiifu na wanyenyekevu, wanaotubia, wenye kufanya ‘ibaadah, wanaofunga Swiyaam au wanaohajiri kwa ajili ya Allaah, wajane, na walio bikra.
[Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]