025-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Furqaan Aayah 27-29: وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
025-Suwrah Al-Furqaan Aayah 27 - 29
Kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا ﴿٢٧﴾ يَا وَيْلَتَىٰ لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا ﴿٢٨﴾ لَّقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي ۗ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلْإِنسَانِ خَذُولًا ﴿٢٩﴾
Na siku dhalimu atakapotafuna mikono yake akisema: Laiti ningeshika njia pamoja na Rasuli. Ee ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki mwandani. Kwa yakini amenipoteza mbali na Ukumbusho baada ya kunijia. Na shaytwaan kwa insani daima ni mwenye kutelekeza. [Al-Furqaan (25): 27, 28, 29]
Sababun-Nuzuwl:
عن ابن عباس رضي الله عنهما أن أبا مُعَيط - وهو عقبة بن أبي معيط - كان يَجلِسُ مع النبي صلى الله عليه وسلم بمكةَ لا يُؤذيه، وكان رجلاً حليمًا، وكان بقيَّةُ قريشٍ إذا جَلَسوا آذَوْه، وكان لأبي مُعيطٍ خليلٌ غائبٌ عنه بالشام (هو أبي بن خلف الجمحي) فقالت قريشٌ: صَبَأَ أبو مُعَيط. وقدِم خليلُه من الشام ليلاً، فقال لامرأته: ما فَعَل محمدٌ مما كان عليه؟ فقالت: أشدُّ مما كان أمرًا. فقال: ما فَعَل خليلي أبو مُعَيط؟ فقالت: صبَأ. فبات بليلةِ سَوءٍ، فلما أصبَح أتاه أبو مُعَيط فحَيَّاه، فلم يرُدَّ عليه التحيةَ، فقال: ما لكَ لا تَرُدُّ عليَّ تحيتي؟ فقال: كيف أَرُدُّ عليك تحيَّتَك وقد صَبَوتَ؟ قال: أَوَ قَدْ فَعَلَتْها قريش؟ قال: نعم. قال: فما يُبرئُ صُدورَهم إِنْ أنا فعلتُ؟ قال: تأتيه في مَجلِسِه فتبزُقُ في وجهه، وتشتُمُه بأخبثِ ما تعلمُ من الشَّتْم. ففعل، فلم يَزد النبيُّ صلى الله عليه وسلم على أن مَسَح وجهه من البُزاق، ثم التفت إليه فقال: "إِنْ وَجَدْتُكَ خَارِجًا مِنْ جِبَالِ مَكَّةَ أَضْرِبُ عُنُقَكَ صَبْرًا" فلمَّا كان يومُ بدرٍ وخَرَج أصحابُه، أبى أن يخرجَ، فقال له أصحابه: اخرجْ معنا. قال: قد وَعَدَني هذا الرجل إن وَجَدَني خارجًا من جبال مكةَ أن يضربَ عُنُقي صبرًا. فقالوا: لك جَمَلٌ أحمرُ لا يُدْرَك، فلو كانتِ الهزيمةُ طِرْتَ عليه، فخرج معهم، فلما هَزَم اللهُ المشركين، وَحَلَ به جَمَلُه في جَدَدٍ من الأرض، فأخذه رسولُ الله صلى الله عليه وسلم أسيرًا في سبعينَ مِن قُرَيْش، وقدِم إليه أبو مُعَيط، فقال: أتقتلُني مِن بين هؤلاء؟ قال: "نَعَمْ، بِمَا بَزَقْتَ فِي وَجْهِي". فأنزل الله في أبي مُعَيْط: ((وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَى يَدَيْهِ)) إلى قوله: ((وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلإِنسَانِ خَذولاً ))
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) kuwa Abu Mu’aytw alikuwa akikaa majilisi pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) mjini Makkah bila kumfanyia maudhi wala vitimbi vyovyote. Alikuwa mtu mkarimu, mpole na mwenye kujiheshimu. Lakini Maquraysh wengine walikuwa wakimuudhi na kumtaabisha sana Rasuli wanapokaa pamoja naye. Abu Mu’aytw alikuwa na rafiki yake mwandani (Ubayya bin Khalaf Al-Jumahiy) ambaye alikuwa amesafiri kwenda Sham. (Na kutokana na kukaa kwake vyema pamoja na Rasuli bila kumfanyia bughudha) Maquraysh walisema: Abu Mu’aytw ameiacha Dini yake (na kufuata dini ya Muhammad). Rafiki yake mwandani (Ubayya bin Khalaf Al-Jumahiy) akarudi toka Sham usiku, na akamuuliza mkewe kuhusu nini kafanya Muhammad kukabiliana na mizengwe na vitimbi anavyofanyiwa. Akamjibu kuwa mambo yamezidi kuliko yalivyokuwa. Akamuuliza: Na vipi rafiki yangu kipenzi Abu Mu’aytw? Akamwambia: Ameacha Dini yake. Akalala usiku mbaya kabisa. Kulipopambazuka, Abu Mu’aytw alimwendea, akamsalimia lakini hakumjibu salaam yake. Akamuuliza: Kunani? Mbona hunijibu salaam yangu? Akamwambia: Vipi nitakujibu salaam yako na wewe ushaacha dini yako? Akamuuliza: Je, Maquraysh pia wameamua hivi? Nifanye jambo gani ili waniridhie? Akamwambia: Nenda kwenye majilisi yake, umtemee mate usoni, kisha mtukane matusi yote machafu ya nguoni unayoyajua. Akaenda na kutekeleza hilo. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) hakujibisha lolote zaidi ya kuyafuta mate usoni mwake, akamgeukia na kumwambia: Nikikupata nje ya milima ya Makkah, basi nitakukata shingo baada ya kukuteka na kukufunga kwenye kigogo. Na siku ya (vita vya) Badr ilipowadia, na wenzake wakajitayarisha kutoka, yeye alikataa kutoka nao. Masahibu zake wakamsihi atoke, lakini aliwaambia: Huyu mtu ameniahidi (ahadi ya onyo) kuwa akinikuta nje ya milima ya Makkah, basi atanifyeka shingo baada ya kuniteka na kunifunga. Wakamwambia kuwa watampa ngamia mwekundu ambaye hakamatiki kwa mbio, na kama watashindwa, basi ngamia ataruka naye juu kutokana na kasi yake, hivyo akaamua kutoka nao. Na Allaah Alipowashinda washirikina, na ngamia wake akatuama naye kwenye ardhi tambarare, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) alimchukua kama mateka na kumjumuisha na mateka wengineo sabiini wa Kiquraysh. Abu Mu’aytw akamwendea na kumuuliza: Je, utaniua mimi tu kati ya hawa? Akamwambia: “Na’am, kwa sababu ya kunitemea mate usoni.” Hapo Allaah ‘Azza wa Jalla Akateremsha kumzungumzia Abu Mu’aytw:
وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا ﴿٢٧﴾ يَا وَيْلَتَىٰ لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا ﴿٢٨﴾ لَّقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي ۗ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلْإِنسَانِ خَذُولًا ﴿٢٩﴾
Na siku dhalimu atakapotafuna mikono yake akisema: Laiti ningeshika njia pamoja na Rasuli. Ee ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki mwandani. Kwa yakini amenipoteza mbali na Ukumbusho baada ya kunijia. Na shaytwaan kwa insani daima ni mwenye kutelekeza. [Al-Furqaan (25): 27, 28, 29]
[Katika Ad-Durar Al-Manthuwr Mujallad wa Tano ukurasa wa 68, Ibn Mardawayh na Abu Nu’aym wamekhariji katika Ad-Dalaail kwa Sanad Swahiyh kupitia kwa Sa’iyd bin Jubayr]