062-Asbaabun-Nuzuwl: Al Jumu'ah Aayah 11: وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انْفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
062-Al-Jumu’ah Aayah 11
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu amrisho la Swalaah ya Ijumaa:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٩﴾
9. Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya Swalaah siku ya Ijumaa, kimbilieni kumdhukuru Allaah na acheni kuuza na kununua. Hivyo ni khayr kwenu mkiwa mnajua.
فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّـهِ وَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ﴿١٠﴾
10. Na inapomalizika Swalaah, tawanyikeni katika ardhi, na tafuteni katika fadhila za Allaah, na mdhukuruni Allaah sana ili mpate kufaulu.
وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا ۚ قُلْ مَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ مِّنَ اللَّـهْوِ وَمِنَ التِّجَارَةِ ۚ وَاللَّـهُ خَيْرُ الرَّازِقِينَ﴿١١﴾
11. Na wanapoona tijara au pumbao wanaikimbilia, na wanakuacha umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi kuliko pumbao na tijara, na Allaah ni Mbora wa wenye kuruzuku.
Sababun-Nuzuwl:
حَدَّثَنَا مُعَاوِيَةُ بْنُ عَمْرٍو، قَالَ حَدَّثَنَا زَائِدَةُ، عَنْ حُصَيْنٍ، عَنْ سَالِمِ بْنِ أَبِي الْجَعْدِ، قَالَ حَدَّثَنَا جَابِرُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ بَيْنَمَا نَحْنُ نُصَلِّي مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم إِذْ أَقْبَلَتْ عِيرٌ تَحْمِلُ طَعَامًا، فَالْتَفَتُوا إِلَيْهَا حَتَّى مَا بَقِيَ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم إِلاَّ اثْنَا عَشَرَ رَجُلاً، فَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ: ((وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انْفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا...))
Ametuhadithia Mu’aawiyah bin ‘Amri amesema, ametuhadithia Zaaidah toka kwa Huswayn toka kwa Saalim bin Abiy Al-Ja’ad amesema, ametuhadithia Jaabir bin ‘Abdillaah amesema: Tulipokuwa sisi tunaswali pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) mara uliwasili msafara (wa biashara) umebeba chakula. Wakauendea, na hata hakubakia pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa watu kumi na mbili tu. Ikashuka Aayah hii:
وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا ۚ
11. Na wanapoona tijara au pumbao wanaikimbilia, na wanakuacha umesimama. [Muslim, Kitaabul-Jumu’ah]
Pia,
وَحَدَّثَنَا رِفَاعَةُ بْنُ الْهَيْثَمِ الْوَاسِطِيُّ، حَدَّثَنَا خَالِدٌ، يَعْنِي الطَّحَّانَ عَنْ حُصَيْنٍ، عَنْ سَالِمٍ، وَأَبِي، سُفْيَانَ عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم يَوْمَ الْجُمُعَةِ فَقَدِمَتْ سُوَيْقَةٌ قَالَ فَخَرَجَ النَّاسُ إِلَيْهَا فَلَمْ يَبْقَ إِلاَّ اثْنَا عَشَرَ رَجُلاً أَنَا فِيهِمْ - قَالَ - فَأَنْزَلَ اللَّهُ : ((وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انْفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا)) إِلَى آخِرِ الآيَةِ .
Ametuhadithia Rifaa’at bin Al-Haytham Al-Waasitwiy, ametuhadithia Khaalid, yaani Atw-Twahhaan toka kwa Huswayn toka kwa Saalim na Abiy Sufyaan toka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah amesema: “Tulikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) siku ya Ijumaa, ukawasili msafara wa mali. Wakatoka watu kuufuatia, na hawakubaki isipokuwa wanaume kumi na mbili, mimi nikiwemo. Hapo Allaah Akateremsha:
وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا ۚ قُلْ مَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ مِّنَ اللَّـهْوِ وَمِنَ التِّجَارَةِ ۚ وَاللَّـهُ خَيْرُ الرَّازِقِينَ﴿١١﴾
Na wanapoona tijara au pumbao wanaikimbilia, na wanakuacha umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi kuliko pumbao na tijara, na Allaah ni Mbora wa wenye kuruzuku.
[Muslim, Kitaab Al-Jumu’ah]
Pia,
حَدَّثَنَا طَلْقُ بْنُ غَنَّامٍ، حَدَّثَنَا زَائِدَةُ، عَنْ حُصَيْنٍ، عَنْ سَالِمٍ، قَالَ حَدَّثَنِي جَابِرٌ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ بَيْنَمَا نَحْنُ نُصَلِّي مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم إِذْ أَقْبَلَتْ مِنَ الشَّأْمِ عِيرٌ، تَحْمِلُ طَعَامًا، فَالْتَفَتُوا إِلَيْهَا، حَتَّى مَا بَقِيَ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم إِلاَّ اثْنَا عَشَرَ رَجُلاً فَنَزَلَتْ: ((وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انْفَضُّوا إِلَيْهَا))
Ametuhadithia Twalq bin Ghannaam, ametuhadithia Zaaidah toka kwa Huswayn toka kwa Saalim amesema, amenihadithia Jaabir ((رضي الله عنه) amesema: Tulipokuwa tunaswali pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) mara ukawasili msafara wa biashara toka Shaam wenye shehena ya chakula, watu wakaufuata hata hakubakia na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa wanaume kumi na mbili. Hapo ikashuka:
وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا
Na wanapoona tijara au pumbao wanaikimbilia,
[Kitaabul-Buyuw’]
Pia,
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُثَنَّى، وَابْنُ، بَشَّارٍ قَالاَ حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ جَعْفَرٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُرَّةَ، عَنْ أَبِي عُبَيْدَةَ، عَنْ كَعْبِ بْنِ عُجْرَةَ، قَالَ دَخَلَ الْمَسْجِدَ وَعَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ أُمِّ الْحَكَمِ يَخْطُبُ قَاعِدًا فَقَالَ انْظُرُوا إِلَى هَذَا الْخَبِيثِ يَخْطُبُ قَاعِدًا وَقَالَ اللَّهُ تَعَالَى: ((وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انْفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا))
Ametuhadithia Muhammad bin Al-Muthannaa na Ibn Bash-shaar wamesema, ametuhadithia Muhammad bin Ja’afar, ametuhadithia Shu’ubah toka kwa Manswuwr toka kwa ‘Amri bin Murrah toka kwa Abiy ‘Ubaydah toka kwa Ka’ab bin ‘Ujrah amesema: Aliingia Msikitini na ‘Abdur-Rahmaan bin Ummi Al-Hakam akiwa anakhutubu akiwa amekaa. Akasema: Mwangalieni khabithi huyu anakhutubu akiwa amekaa na Allaah Ta’alaa Amesema:
وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا ۚ قُلْ مَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ مِّنَ اللَّـهْوِ وَمِنَ التِّجَارَةِ ۚ وَاللَّـهُ خَيْرُ الرَّازِقِينَ﴿١١﴾
Na wanapoona tijara au pumbao wanaikimbilia, na wanakuacha umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi kuliko pumbao na tijara, na Allaah ni Mbora wa wenye kuruzuku.
[Muslim, Kitaabul-Jumu’ah]
Pia,
Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah amesema: Walikuwa wanapofungishwa nikaah, wanapita na magoma na zumari na wanamwacha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesimama juu ya mimbari, na wanaondoka na kutawanyika. Hapo Allaah Akateremsha:
وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا ۚ
Na wanapoona tijara au pumbao wanaikimbilia, na wanakuacha umesimama.
[At-Twabariy ameikhariji Sanadi ya wapokezi wake ambao ni waaminifu na Abuu ‘Awaanah katika Swahiyh yake. Kama alivyoisema Al-Haafidh katika Al-Fat-h mjeledi wa tatu ukurasa wa 76]
Imekuja katika Tafsiyr ya Ibn Jariyj na katika Al-Fat-h ya kuwa walipokuwa wakifungishwa nikaah, vijakazi hupiga zumari na watu wakavutika kwao na kumwacha Rasuli wa Allaah amesimama, na hapo ikashuka Aayah hii.
Na katika kitabu cha Ad-Durru Al-Manthuwr mjeledi wa sita ukurasa 221 ni kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anawakhutubia watu Siku ya Ijumaa. Kama ni nikaah, watu wake hucheza na hupita kwa burudani kwenye Msikiti, na kama ni msafara wa biashara, hushukia Al-Batwhaa. Al-Batwhaa ilikuwa ni uwanja wa Msikiti jirani na Baqiy Al-Gharqad. Mabedui walikuwa wanapoleta farasi, ngamia, mbuzi, kondoo na bidhaa za Mabedui, hushukia Al-Batwhaa. Wanaposikia hilo waliokaa kwa ajili ya khutbah, hunyanyuka kwenda kwenye pumbao na biashara, na humwacha (Rasuli) amesimama. Na hapo Allaah Akawakemea Waumini kwa ajili ya Nabiy Wake (Swalla Allaah álayhi wa aalihii wa Sallam Akasema:
وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا ۚ
11. Na wanapoona tijara au pumbao wanaikimbilia, na wanakuacha umesimama.