041-Asbaabun-Nuzuwl: Fusw-Swilat Aayah 22: وَمَا كُنْتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَنْ يَشْهَدَ، عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
041-Asbaabun-Nuzuwl Fusw-Swilat Aayah 22
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَـٰكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ اللَّـهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ﴿٢٢﴾
Na hamkuwa mkijisitiri hata yasishuhudie masikio yenu, na wala macho yenu, na wala ngozi zenu; lakini mlidhania kwamba Allaah Hajui mengi katika yale mnayoyatenda. [Fusswilat (41:22)]
Sababun-Nuzuwl:
حَدَّثَنَا الصَّلْتُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ زُرَيْعٍ، عَنْ رَوْحِ بْنِ الْقَاسِمِ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، عَنْ أَبِي مَعْمَرٍ، عَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ ((وَمَا كُنْتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَنْ يَشْهَدَ، عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ)) الآيَةَ - كَانَ رَجُلاَنِ مِنْ قُرَيْشٍ وَخَتَنٌ لَهُمَا مِنْ ثَقِيفَ، أَوْ رَجُلاَنِ مِنْ ثَقِيفَ وَخَتَنٌ لَهُمَا مِنْ قُرَيْشٍ فِي بَيْتٍ فَقَالَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ أَتُرَوْنَ أَنَّ اللَّهَ يَسْمَعُ حَدِيثَنَا قَالَ بَعْضُهُمْ يَسْمَعُ بَعْضَهُ. وَقَالَ بَعْضُهُمْ لَئِنْ كَانَ يَسْمَعُ بَعْضَهُ لَقَدْ يَسْمَعُ كُلَّهُ. فَأُنْزِلَتْ ((وَمَا كُنْتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَنْ يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلاَ أَبْصَارُكُمْ)) الآية
Ametuhadithia Asw-Swalt bin Muhammad, ametuhadithia Yaziyd bin Zuray‘i, toka kwa Rawh bin Al-Qaasim, toka kwa Manswuwr, toka kwa Mujaahid, toka kwa Abu Mu’ammar, toka kwa Ibn Mas‘uwd amesema:
وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ
Na hamkuwa mkijisitiri hata yasishuhudie masikio yenu. [Fusswilat (41:22)]
Maquraysh wawili pamoja na shemeji yao toka Thaqiyf –au watu wawili toka Thaqiyf na shemeji yao Mquraysh- walikuwa katika nyumba (wakizungumza yasiyomridhisha Allah). (Halafu) wakaulizana: Hivi mnadhani kwamba Allaah Anasikia mazungumzo yetu? Baadhi yao wakasema: Anasikia sehemu ya mazungumzo. Na wengine wakasema: Ikiwa Anasikia sehemu ya mazungumzo, basi kwa hakika Anayasikia yote. Na hapo ikateremshwa:
وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ
Na hamkuwa mkijisitiri hata yasishuhudie masikio yenu, na wala macho yenu. [Fussilat: 41:22)]
[Al-Bukhaariy Mujallad 10 Uk. 182]
Al-Bukhaariy ameirudia Hadiyth hii katika Mujallad wa 17 Uk. 276. Na Muslim ameikhariji katika Mujallad wa 17 Uk. 122. Pia At-Tirmidhiy ameikhariji katika Mujallad wa 4 Uk. 178 kwa Isnaad mbili, moja amesema ni Swahiyh na nyingine amesema ni Hasan.
Wengine walioikhariji ni Ahmad katika Mujallad wa 1 Kurasa 381, 408, 426, 442 na 444, At-Twayaalsiy katika Mujallad 2 Uk. 23, Ibn Jariyr katika Mujallad wa 24 Uk. 109, Al-Bayhaqiy katika “Al-Asmaa was Swifaat” Mujallad wa 1 Uk. 177 na At-Twahaawiy katika Mujallad 1 Uk. 37 katika “Mushkil Al-Aathaar”.
Katika baadhi ya Asaaniyd zake katika “As-Swahiyh” na kwenye vitabu vingine, Hadiyth inasema: “Mmoja wao akasema: Je, mnadhani kwamba Allaah Anasikia maneno yetu? Mwingine akasema: Sisi tukinyanyua sauti zetu basi Anazisikia, na kama hatunyanyui basi Hasikii. Wengine wakasema: Kama Anasikia sehemu ya sauti, basi Anaisikia yote. Amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaelezwa hilo, na Allaah (عز وجل) Akateremsha Aayah.”