024-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nuwr Aayah 03: الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

 

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

24- Suwrah An-Nuwr Aayah 3

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ ﴿٣﴾

Mwanamme mzinifu hafungi nikaah isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina; na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamme mzinifu au mshirikina. Na imeharamishwa hivyo kwa Waumini. [An Nuwr (24:3)]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا عَبْدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا رَوْحُ بْنُ عُبَادَةَ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ الأَخْنَسِ، أَخْبَرَنِي عَمْرُو بْنُ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، قَالَ كَانَ رَجُلٌ يُقَالُ لَهُ مَرْثَدُ بْنُ أَبِي مَرْثَدٍ وَكَانَ رَجُلاً يَحْمِلُ الأَسْرَى مِنْ مَكَّةَ حَتَّى يَأْتِيَ بِهِمُ الْمَدِينَةَ قَالَ وَكَانَتِ امْرَأَةٌ بَغِيٌّ بِمَكَّةَ يُقَالُ لَهَا عَنَاقُ وَكَانَتْ صَدِيقَةً لَهُ وَإِنَّهُ كَانَ وَعَدَ رَجُلاً مِنْ أُسَارَى مَكَّةَ يَحْمِلُهُ قَالَ فَجِئْتُ حَتَّى انْتَهَيْتُ إِلَى ظِلِّ حَائِطٍ مِنْ حَوَائِطِ مَكَّةَ فِي لَيْلَةٍ مُقْمِرَةٍ ‏.‏ قَالَ فَجَاءَتْ عَنَاقُ فَأَبْصَرَتْ سَوَادَ ظِلِّي بِجَنْبِ الْحَائِطِ فَلَمَّا انْتَهَتْ إِلَىَّ عَرَفَتْهُ فَقَالَتْ مَرْثَدُ فَقُلْتُ مَرْثَدُ ‏.‏ فَقَالَتْ مَرْحَبًا وَأَهْلاً هَلُمَّ فَبِتْ عِنْدَنَا اللَّيْلَةَ ‏.‏ قَالَ قُلْتُ يَا عَنَاقُ حَرَّمَ اللَّهُ الزِّنَا ‏.‏ قَالَتْ يَا أَهْلَ الْخِيَامِ هَذَا الرَّجُلُ يَحْمِلُ أَسْرَاكُمْ ‏.‏ قَالَ فَتَبِعَنِي ثَمَانِيَةٌ وَسَلَكْتُ الْخَنْدَمَةَ فَانْتَهَيْتُ إِلَى كَهْفٍ أَوْ غَارٍ فَدَخَلْتُ فَجَاءُوا حَتَّى قَامُوا عَلَى رَأْسِي فَبَالُوا فَطَلَّ بَوْلُهُمْ عَلَى رَأْسِي وَأَعْمَاهُمُ اللَّهُ عَنِّي ‏.‏ قَالَ ثُمَّ رَجَعُوا وَرَجَعْتُ إِلَى صَاحِبِي فَحَمَلْتُهُ وَكَانَ رَجُلاً ثَقِيلاً حَتَّى انْتَهَيْتُ إِلَى الإِذْخِرِ فَفَكَكْتُ عَنْهُ كَبْلَهُ فَجَعَلْتُ أَحْمِلُهُ وَيُعِينُنِي حَتَّى قَدِمْتُ الْمَدِينَةَ فَأَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَنْكِحُ عَنَاقًا مَرَّتَيْنِ فَأَمْسَكَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَلَمْ يَرُدَّ عَلَىَّ شَيْئًا حَتَّى نَزَلَتِ ‏:‏ ((الزَّانِي لاَ يَنْكِحُ إِلاَّ زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لاَ يَنْكِحُهَا إِلاَّ زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ وَحُرِّمَ ذَلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ ‏))  فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ يَا مَرْثَدُ الزَّانِي لاَ يَنْكِحُ إِلاَّ زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لاَ يَنْكِحُهَا إِلاَّ زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ فَلاَ تَنْكِحْهَا ‏"‏ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ لاَ نَعْرِفُهُ إِلاَّ مِنْ هَذَا الْوَجْهِ ‏.‏

 

Ametuhadithia ‘Abdu bin Humayd, ametuhadithia Rawh bin ‘Ubaadah toka kwa ‘Ubaydullaa bin Al-Akhnas amesema: Amenieleza ‘Amri bin Shu’ayb akipokea toka kwa baba yake toka kwa babu yake aliyesema: Kulikuwa na mtu ajulikanaye kama Marthad. Kazi yake ilikuwa ni kuwabeba na kuwatorosha mateka toka Makkah kuwaleta Madiynah. Na hapo Makkah alikuwepo mwanamke kahaba aitwaye ‘Anaaq ambaye alikuwa ni hawara yake Marthad (kabla hajasilimu). Marthad alikuwa amemwahidi mtu mmoja katika mateka wa Makkah kuwa atambeba (kumtorosha). [Marthad anasema]: Nikaja hadi nikaishilia katika kivuli cha kuta kati ya kuta za Makkah katika usiku angavu wa nuru ya mwezi. ‘Anaaq akaja, akaona weusi wa kivuli changu pembeni ya ukuta. Aliponifikia, alinitambua akasema: Ni Marthad! Nami nikasema ni (mimi) Marthad. Akasema: Karibu sana, njoo basi ulale kwetu usiku huu. Nikamwambia: Ee ‘Anaaq! Allaah Ameharamisha zinaa! (Hapo hapo) akapiga ukelele na kusema: Enyi watu wa makhema! Huyu hapa mtu anayewatorosha mateka wenu. Watu wanane wakaniandama, nikapita Al-Khandamah, nikakimbilia pangoni na kuingia. Wakaja mpaka wakasimama juu ya kichwa changu (mdomo wa pango) lakini Allaah Aliwaziba macho wasiweze kuniona. Kisha wakaondoka, nami nikarudi kwa mwenzangu, nikambeba, naye alikuwa mzito. Nikamfuata mwingine, nikamfungua minyonyoro yake, nikaanza kumbeba huku akinilemea na kunichosha mpaka nikawasili Madiynah. Nikamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Je, naweza kumwoa ‘Anaaq? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akanyamaza, hakujibu kitu mpaka iliposhuka:

 

الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ ﴿٣﴾

Mwanamme mzinifu hafungi nikaah isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina; na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamme mzinifu au mshirikina. Na imeharamishwa hivyo kwa Waumini. [An Nuwr (24:3)]

 

Na hapo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akamwambia: ((Ee Marthad! Mwanamme mzinifu hafungi nikaah isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina; na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamme mzinifu au mshirikina, basi usimwoe)). [At-Tirmidhiy Mujallad Wa Ukurasa wa 152]

 

Hadiyth hii ni Hasan Ghariyb, haijulikani isipokuwa kwa picha hii.

 

Hadiyth imekharijiwa na Abu Daawuwd katika Mujallad wa Pili ukurasa wa 176, An-Nasaaiy katika Mujallad wa Pili ukurasa wa 54, na Ibn Jariyr katika Mujallad wa Kumi na Nane ukurasa wa 71.

 

 

Share