063-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Munaafiquwn Aayah 1-8: إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ قَالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّـهِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

Al-Munaafiquwn Aayah 1 - 8

 Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى):

إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ قَالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَكَاذِبُونَ﴿١﴾

1. Watakapokujia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wanafiki wakisema: Tunashuhudia kwamba wewe bila shaka ni Rasuli wa Allaah. Na Allaah Anajua kuwa wewe ni Rasuli Wake, na Allaah Anashuhudia kuwa hakika wanafiki ni waongo.

 Na:

هُمُ الَّذِينَ يَقُولُونَ لَا تُنفِقُوا عَلَىٰ مَنْ عِندَ رَسُولِ اللَّـهِ حَتَّىٰ يَنفَضُّوا ۗ وَلِلَّـهِ خَزَائِنُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَفْقَهُونَ﴿٧﴾

7. Wao ndio wale wasemao: Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Rasuli wa Allaah mpaka waondokelee mbali.  Na ilhali ni za Allaah Pekee hazina za mbingu na ardhi, lakini wanafiki hawafahamu.

يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعْنَا إِلَى الْمَدِينَةِ لَيُخْرِجَنَّ الْأَعَزُّ مِنْهَا الْأَذَلَّ ۚ وَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ﴿٨﴾

8. Wanasema: Tutakaporudi Madiynah, mwenye hadhi zaidi bila shaka atamfukuza humo aliye dhalili. Na ilhali utukufu ni wa Allaah na wa Rasuli Wake na wa Waumini, lakini wanafiki hawajui.

Sababun-Nuzuwl:

عَنْ زَيْدِ بْنِ أَرْقَمَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ كُنْتُ مَعَ عَمِّي فَسَمِعْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ أُبَىٍّ ابْنَ سَلُولَ يَقُولُ لاَ تُنْفِقُوا عَلَى مَنْ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ حَتَّى يَنْفَضُّوا‏.‏ وَقَالَ أَيْضًا لَئِنْ رَجَعْنَا إِلَى الْمَدِينَةِ لَيُخْرِجَنَّ الأَعَزُّ مِنْهَا الأَذَلَّ‏.‏ فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لِعَمِّي فَذَكَرَ عَمِّي لِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَأَرْسَلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِلَى عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أُبَىٍّ وَأَصْحَابِهِ، فَحَلَفُوا مَا قَالُوا، فَصَدَّقَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَكَذَّبَنِي، فَأَصَابَنِي هَمٌّ لَمْ يُصِبْنِي مِثْلُهُ، فَجَلَسْتُ فِي بَيْتِي، فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: ((إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ‏))‏ إِلَى قَوْلِهِ: ((‏هُمُ الَّذِينَ يَقُولُونَ لاَ تُنْفِقُوا عَلَى مَنْ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ‏)) ‏ إِلَى قَوْلِهِ: ((‏لَيُخْرِجَنَّ الأَعَزُّ مِنْهَا الأَذَلَّ‏))‏ فَأَرْسَلَ إِلَىَّ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَرَأَهَا عَلَىَّ ثُمَّ قَالَ ‏"‏ إِنَّ اللَّهَ قَدْ صَدَّقَكَ ‏"‏‏.‏

Zaid bin Arqam (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Nilipokuwa pamoja na ‘Ammi yangu nilimsikia ‘Abdullaah bin Ubayy Ibn Masluwl (Mnafiki mkuu) akisema:  Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Rasuli wa Allaah mpaka waondokelee mbali.” Na akasema pia: “Tutakaporudi Madiynah, mwenye hadhi zaidi atamfukuza humo aliye dhalili.” Nikamtajia  hayo ‘Ammi yangu na ‘Ammi yangu akamwelezea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akamwita ‘Abdullaah ibn Ubayy na Maswahaba zake (kuwauliza), wakaapa kuwa hawakusema hivyo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akawasadikisha na badala yake akanikadhibisha. Ikanigubika ghamu ambayo sikuwahi kuipata mfano wake. Nikabakia nyumbani kwangu (kuogopa nisiitwe muongo) kisha hapo Allaah (عزّ وجلّ) Akateremsha:

إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ قَالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّـهِ ۗ  

Watakapokujia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wanafiki wakisema: Tunashuhudia kwamba wewe bila shaka ni Rasuli wa Allaah.

Mpaka kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

هُمُ الَّذِينَ يَقُولُونَ لَا تُنفِقُوا عَلَىٰ مَنْ عِندَ رَسُولِ اللَّـهِ حَتَّىٰ يَنفَضُّوا ۗ وَلِلَّـهِ خَزَائِنُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَفْقَهُونَ﴿٧﴾

7. Wao ndio wale wasemao: Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Rasuli wa Allaah mpaka waondokelee mbali.  Na ilhali ni za Allaah Pekee hazina za mbingu na ardhi, lakini wanafiki hawafahamu.

Mpaka kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

  لَيُخْرِجَنَّ الْأَعَزُّ مِنْهَا الْأَذَلَّ ۚ  

mwenye hadhi zaidi bila shaka atamfukuza humo aliye dhalili.  

Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akaniita na kunisomea kisha akasema:  ((Allaah Amesadikisha kauli yako)). [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]

Riwaayah nyengine ni kama ifuatavyo: (pamoja na Aayah zinazohusiana na kisa hicho)

عن زَيْدِ بْنِ أَرْقَمَ، قَالَ كُنْتُ مَعَ عَمِّي فَسَمِعْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ أُبَىٍّ ابْنَ سَلُولَ، يَقُولُ لاَ تُنْفِقُوا عَلَى مَنْ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ حَتَّى يَنْفَضُّوا، وَلَئِنْ رَجَعْنَا إِلَى الْمَدِينَةِ لَيُخْرِجَنَّ الأَعَزُّ مِنْهَا الأَذَلَّ‏.‏ فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لِعَمِّي، فَذَكَرَ عَمِّي لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ‏{‏فَدَعَانِي فَحَدَّثْتُهُ، فَأَرْسَلَ إِلَى عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أُبَىٍّ وَأَصْحَابِهِ فَحَلَفُوا مَا قَالُوا، وَكَذَّبَنِي النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم‏}‏ وَصَدَّقَهُمْ، فَأَصَابَنِي غَمٌّ لَمْ يُصِبْنِي مِثْلُهُ قَطُّ، فَجَلَسْتُ فِي بَيْتِي وَقَالَ عَمِّي مَا أَرَدْتَ إِلَى أَنْ كَذَّبَكَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم وَمَقَتَكَ‏.‏ فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى: ((‏إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ قَالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّهِ‏))‏ وَأَرْسَلَ إِلَىَّ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَقَرَأَهَا وَقَالَ ‏"‏ إِنَّ اللَّهَ قَدْ صَدَّقَكَ ‏"‏‏.‏

Zaid bin Arqam (رضي الله عنه)  amehadithia kwamba: Nilipokuwa pamoja na ‘Ammi yangu nilimsikia ‘Abdullaah bin Ubayy Ibn Masluwl (Mnafiki mkuu) akisema:  Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Rasuli wa Allaah mpaka waondokelee mbali. Na tutakaporudi Madiynah, mwenye hadhi zaidi atamfukuza humo aliye dhalili.” Nikamtajia  hayo ‘Ammi yangu, naye ‘Ammi wangu akamtajia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akaniita nikamhadithia, naye akamwita ‘Abdullaah ibn Ubayy na Maswahaba zake (kuwauliza), wakaapa kuwa hawakusema hivyo.  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akanikadhibisha na badala yake akawasadikisha wao. Basi ikanigubika ghamu ambayo sikuwahi kuipata mfano wake. Nikabakia nyumbani (kuogopa kuitwa mwongo), na ‘Ammi yangu akaniambia: “Wewe hukukusudia kutaka  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akukadhibishe na akughadhibikie”  Hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:  

 إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ قَالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّـهِ ۗ

Watakapokujia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wanafiki wakisema: Tunashuhudia kwamba wewe bila shaka ni Rasuli wa Allaah.

Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniita na akaisoma kisha akasema: ((Allaah Amesadikisha kauli yako)) [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]

Aayah zinazohusiana katika Suwrah hiyo ya Al-Munaafiquwn (Wanafiki) ni:

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ قَالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَكَاذِبُونَ﴿١﴾

1. Watakapokujia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wanafiki wakisema: Tunashuhudia kwamba wewe bila shaka ni Rasuli wa Allaah. Na Allaah Anajua kuwa wewe ni Rasuli Wake, na Allaah Anashuhudia kuwa hakika wanafiki ni waongo.

اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٢﴾

2. Wamefanya viapo vyao kuwa ni ngao, hivyo wakazuia kufuata njia ya Allaah, hakika ni maovu mno waliyokuwa wakiyatenda.

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا فَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَفْقَهُونَ﴿٣﴾

3. Hiyo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru, basi ikapigwa mhuri juu ya nyoyo zao kwa hiyo hawafahamu lolote.

وَإِذَا رَأَيْتَهُمْ تُعْجِبُكَ أَجْسَامُهُمْ ۖ وَإِن يَقُولُوا تَسْمَعْ لِقَوْلِهِمْ ۖ كَأَنَّهُمْ خُشُبٌ مُّسَنَّدَةٌ ۖ يَحْسَبُونَ كُلَّ صَيْحَةٍ عَلَيْهِمْ ۚ هُمُ الْعَدُوُّ فَاحْذَرْهُمْ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّـهُ ۖ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٤﴾

4. Na unapowaona, inakupendezesha miili yao, na wanaposema, unasikiliza kauli zao. Lakini wao ni kama magogo yaliyoegemezwa; wandhania kuwa kila ukelele unaopigwa ni kwa ajili yao. Hao ndio maadui, basi tahadhari nao, Allaah Awaangamizilie mbali; namna gani wanavyoghilibiwa!

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا يَسْتَغْفِرْ لَكُمْ رَسُولُ اللَّـهِ لَوَّوْا رُءُوسَهُمْ وَرَأَيْتَهُمْ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ﴿٥﴾

5. Wanapoambiwa: Njooni ili Rasuli wa Allaah akuombeeni maghfirah. Hupindisha vichwa vyao, na utawaona wanakwepa na huku wao ni wenye kutakabari.

سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَسْتَغْفَرْتَ لَهُمْ أَمْ لَمْ تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ لَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٦﴾

6. Ni sawasawa juu yao, ukiwaombea maghfirah au usiwaombee, Allaah Hatowaghufuria kamwe. Hakika Allaah Haongoi watu mafasiki.

Share