024-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nuwr Aayah 61: لَّيْسَ عَلَى الْأَعْمَىٰ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْمَرِيضِ حَرَجٌ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

024-Suwrah An-Nuwr Aayah 61

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

لَّيْسَ عَلَى الْأَعْمَىٰ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْمَرِيضِ حَرَجٌ وَلَا عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَن تَأْكُلُوا مِن بُيُوتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ آبَائِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أُمَّهَاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ إِخْوَانِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَخَوَاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَعْمَامِكُمْ أَوْ بُيُوتِ عَمَّاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَخْوَالِكُمْ أَوْ بُيُوتِ خَالَاتِكُمْ أَوْ مَا مَلَكْتُم مَّفَاتِحَهُ أَوْ صَدِيقِكُمْ ۚ لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَأْكُلُوا جَمِيعًا أَوْ أَشْتَاتًا ۚ فَإِذَا دَخَلْتُم بُيُوتًا فَسَلِّمُوا عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ تَحِيَّةً مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُبَارَكَةً طَيِّبَةً ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٦١﴾

Si vibaya kwa kipofu, na wala si vibaya kwa kilema, na wala si vibaya kwa mgonjwa, na wala nyinyi wenyewe kama mtakula majumbani mwenu, au majumbani mwa baba zenu, au majumbani mwa mama zenu, au majumbani mwa kaka zenu, au majumbani mwa dada zenu, au majumbani mwa ‘ammi zenu, au majumbani mwa shangazi zenu, au majumbani mwa wajomba zenu, au majumbani mwa makhalati zenu au za mliowashikia funguo zao, au rafiki yenu. Hakuna ubaya kama mkila pamoja au mbali mbali. Mtakapoingia majumbani toleaneni salaam; maamkizi kutoka kwa Allaah, yenye Baraka, mazuri. Hivyo ndivyo Anavyokubainishieni Allaah Aayaat ili mpate kutia akilini. [An-Nuwr:  61]

Sababun-Nuzuwl: 

حدثنا زيد بن أخزم أبو طالب الطائي ثنا بشر بن عمر ثنا إبراهيم بن سعد عن صالح بن كيسان عن الزهري عن عروة عن عائشة قالت كانَ المسلِمونَ يرغبونَ في النَّفيرِ معَ رسولِ اللَّهِ - صلَّى اللَّه عليهِ وعلى آلِهِ وسلَّمَ - فَيدفعونَ مفاتحَهُم إلى ضُمَنائِهِم ويقولونَ لَهُم: قد أحلَلنا لَكُم أن تأكُلوا ما أحببتُمْ، فَكانوا يقولونَ: إنَّهُ لا يحلُّ لَنا، أنَّهم أذِنوا عن غَيرِ طيبِ نفسٍ. فأنزلَ اللَّهُ - عزَّ وجلَّ :  لَّيْسَ عَلَى الْأَعْمَىٰ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْمَرِيضِ حَرَجٌ وَلَا عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَن تَأْكُلُوا مِن بُيُوتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ آبَائِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أُمَّهَاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ إِخْوَانِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَخَوَاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَعْمَامِكُمْ أَوْ بُيُوتِ عَمَّاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَخْوَالِكُمْ أَوْ بُيُوتِ خَالَاتِكُمْ أَوْ مَا مَلَكْتُم مَّفَاتِحَهُ أَوْ صَدِيقِكُمْ ۚ  

Ametuhadithia Zayd bin Akhzam Abu Twaalib At-Twaaiy, ametuhadithia Bishr bin ‘Umar, ametuhadithia Ibraahiym bin Sa’ad toka kwa Swaalih bin Kiysaan toka kwa Az-Zuhriy toka kwa ‘Urwah toka kwa  ‘Aaishah amesema: Waislamu walipotaka kutoka kuitikia mbiu ya mgambo ya kujitayarisha kwenda vitani pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), waliacha funguo za nyumba zao kwa wasimamizi wao na kuwaambia: Tumewaruhusuni kula mvipendavyo humo. Lakini wao [wasimamizi] walisema: Si halali kwetu kula, kwa kuwa wameturuhusu kula bila roho safi. Na hapo ndipo iliposhuka Kauli Yake Ta’aalaa:

لَّيْسَ عَلَى الْأَعْمَىٰ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْمَرِيضِ حَرَجٌ وَلَا عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَن تَأْكُلُوا مِن بُيُوتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ آبَائِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أُمَّهَاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ إِخْوَانِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَخَوَاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَعْمَامِكُمْ أَوْ بُيُوتِ عَمَّاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَخْوَالِكُمْ أَوْ بُيُوتِ خَالَاتِكُمْ أَوْ مَا مَلَكْتُم مَّفَاتِحَهُ أَوْ صَدِيقِكُمْ ۚ  

Si vibaya kwa kipofu, na wala si vibaya kwa kilema, na wala si vibaya kwa mgonjwa, na wala nyinyi wenyewe kama mtakula majumbani mwenu, au majumbani mwa baba zenu, au majumbani mwa mama zenu, au majumbani mwa kaka zenu, au majumbani mwa dada zenu, au majumbani mwa ‘ammi zenu, au majumbani mwa shangazi zenu, au majumbani mwa wajomba zenu, au majumbani mwa makhalati zenu au za mliowashikia funguo zao, au rafiki yenu.

[Imaam Ahmad bin ‘Amri bin ‘Abdul Khaaliq almaarufu kama Al-Bazzaar kama ilivyo katika Kashf Al-Astaar Mujallad wa Tatu ukurasa wa 61, wapokezi wake ni wapokezi As-Swawhiyh, Na As-Suyuutwiy katika Lubaab An-Nuquwl amesema kuwa Sanad yake ni Swahiyh]

Na pia,

  أخبرنا الحسن بن محمد الفارسي قال: أخبرنا محمد بن عبد الله بن الفضل التاجر قال: أخبرنا أحمد بن محمد بن الحسن الحافظ قال: أخبرنا محمد بن يحيى قال: أخبرنا إسماعيل ابن أبى أويس قال: حدثني مالك عن ابن شهاب عن سعيد ابن المسيب أنه كان يقول في هذه الآية: نزلت في أناس كانوا إذا خرجوا مع النبي صلى الله عليه وسلم وضعوا مفاتيح بيوتهم عند الاعمى والاعرج والمريض وعند أقاربهم، وكانوا يأمرونهم أن يأكلوا مما في بيوتهم إذا احتاجوا إلى ذلك، وكانوا يتقون أن يأكلوا منها ويقولون: نخشى أن لا تكون أنفسهم بذلك طيبة، فأنزل الله تعالى هذه الآية.

Al-Hasan bin Muhammad Al-Faarisiy amesema: Ametueleza Muhammad bin ‘Abdallah bin Al-Fadhl At-Taajir [Mfanyibiashara] akisema: Ametueleza Ahmad bin Muhammad bin Al-Hasan Al-Haafidh, ametueleza Muhammad bin Yahyaa amesema: Ametueleza Ismaa’iyl bin Abiy Uways amesema: Amenihadithia Maalik toka kwa Ibn Shihaab toka kwa Sa’iyd bin Al-Musayyib kwamba alikuwa anasema kuhusiana na Aayah hii, iliteremshwa kuwazungumzia watu ambao walikuwa wanapotoka pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), huweka funguo za nyumba zao kwa kipofu, au kwa kiwete, au kwa mgonjwa, au kwa jamaa zao. Walikuwa wakiwaruhusu kula vilivyomo ndani ya nyumba hizo kama watahitaji kufanya hivyo. Lakini watu hao walikuwa wakijizuia kula na kusema: Tunachelea roho zao zisiwe safi kwa hilo. Na hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

Share