025-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Furqaan Aayah 68: وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

025-Asbaab Nuzuwl Al-Furqaan Aayah 68

Kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا 

Na wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha isipokuwa kwa haki, na wala hawazini. Na atakayefanya hivyo atakutana na adhabu. [Al-Furqaan (25:68)]

Sababun-Nuzuwl: 

حَدَّثَنَا قُتَيْبَةُ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ شُرَحْبِيلَ، قَالَ قَالَ عَبْدُ اللَّهِ قَالَ رَجُلٌ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَىُّ الذَّنْبِ أَكْبَرُ عِنْدَ اللَّهِ قَالَ ‏"‏ أَنْ تَدْعُوَ لِلَّهِ نِدًّا، وَهْوَ خَلَقَكَ ‏"‏‏.‏ قَالَ ثُمَّ أَىّ قَالَ ‏"‏ ثُمَّ أَنْ تَقْتُلَ وَلَدَكَ، أَنْ يَطْعَمَ مَعَكَ ‏"‏‏.‏ قَالَ ثُمَّ أَىّ قَالَ ‏"‏ أَنْ تُزَانِيَ حَلِيلَةَ جَارِكَ ‏"‏‏.‏ فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَصْدِيقَهَا ‏((‏وَالَّذِينَ لاَ يَدْعُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ وَلاَ يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ وَلاَ يَزْنُونَ وَمَنْ يَفْعَلْ ذَلِكَ)) الآيَةَ‏.‏

Ametuhadithia Musaddad, ametuhadithia Yahyaa toka kwa Sufyaan amesema, amenihadithia Mansuwr toka kwa Abu Waail toka kwa Abu Maysarah toka kwa ‘Abdullaah amesema, na amenihadithia Waaswil toka kwa Abu Waail toka kwa ‘Abdullaah (Radhwiya Allaah ‘anhu), nilimuuliza, au Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) aliulizwa: Ni dhambi ipi kubwa zaidi mbele ya Allaah? Akasema: Ni kumfanyia Allaah mshirika, na Yeye Amekuumba [Shirki]. Nikamuuliza: Kisha ipi? Akasema: Ni kumuua mwanao kwa kuhofia atakula pamoja nawe [kuhofia umasikini]. Nikamuuliza: Kisha ipi? Akasema: Ni kuzini na mke wa jirani yako. Akasema: Ikateremka Aayah hii kuthibitisha maneno ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam):

وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا 

Na wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha isipokuwa kwa haki, na wala hawazini. Na atakayefanya hivyo atakutana na adhabu. [Al-Furqaan (25:68)]

[Al-Bukhaariy katika Mujallad wa Kumi ukurasa wa 109]

Al-Bukhaariy (Rahimahu-Allaah) ameitaja Hadiyth hii katika mahala kadhaa. Kati ya mahala hapo ni katika Mujallad wa Kumi na Tano ukurasa wa 204 na Mujallad wa Kumi na Saba ukurasa wa 289. Pia Muslim katika Mujallad wa Pili ukurasa wa 80, na At-Tirmidhiy katika Mujallad wa Nne ukurasa wa 157]

Pia Sababun-Nuzuwl:

 عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ـ أَنَّ نَاسًا، مِنْ أَهْلِ الشِّرْكِ كَانُوا قَدْ قَتَلُوا وَأَكْثَرُوا وَزَنَوْا وَأَكْثَرُوا، فَأَتَوْا مُحَمَّدًا صلى الله عليه وسلم فَقَالُوا إِنَّ الَّذِي تَقُولُ وَتَدْعُو إِلَيْهِ لَحَسَنٌ لَوْ تُخْبِرُنَا أَنَّ لِمَا عَمِلْنَا كَفَّارَةً‏.‏ فَنَزَلَ ((‏وَالَّذِينَ لاَ يَدْعُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ وَلاَ يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ وَلاَ يَزْنُونَ‏))  وَنَزَلَ: ((‏قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ لاَ تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ‏))

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) kwamba watu washirikina walikuwa wameua na wameua watu wengi sana, na wamezini na wamezini na wanawake wengi sana. Wakamwendea Muhammad (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) wakamwambia: Hakika haya uyasemayo ni mazuri sana, basi ungetueleza kama kuna kafara kwa hayo tuliyoyafanya. Na hapo ikateremka:

وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا 

Na wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha isipokuwa kwa haki, na wala hawazini. Na atakayefanya hivyo atakutana na adhabu. [Al-Furqaan (25:68)]

Na ikateremka pia:

قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّـهِ

Sema: Enyi waja Wangu ambao wamepindukia mipaka juu ya nafsi zao: Msikate tamaa na Rahmah ya Allaah. [Az-Zumar (39: 53)]. [Al-Bukhaariy katika Mujallad wa Kumi ukurasa wa 170, Muslim katika Mujallad wa Pili ukurasa wa 139 na An-Nasaaiy katika Mujallad wa Saba ukurasa wa 80]

Hakuna kizuizi cha kuwa Aayah ilishuka kwa sababu mbili kwa pamoja. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.

Share