033-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Ahzaab Aayah 37: وَإِذْ تَقُولُ لِلَّذِي أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَأَنْعَمْتَ عَلَيْهِ أَمْسِكْ عَلَيْكَ زَوْجَكَ وَاتَّقِ اللَّـهَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

033-Asbaabun-Nuzuwl Al-Ahzaab Aayah 37

 

 

 

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

وَإِذْ تَقُولُ لِلَّذِي أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَأَنْعَمْتَ عَلَيْهِ أَمْسِكْ عَلَيْكَ زَوْجَكَ وَاتَّقِ اللَّـهَ وَتُخْفِي فِي نَفْسِكَ مَا اللَّـهُ مُبْدِيهِ وَتَخْشَى النَّاسَ وَاللَّـهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَاهُ ۖ فَلَمَّا قَضَىٰ زَيْدٌ مِّنْهَا وَطَرًا زَوَّجْنَاكَهَا لِكَيْ لَا يَكُونَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ حَرَجٌ فِي أَزْوَاجِ أَدْعِيَائِهِمْ إِذَا قَضَوْا مِنْهُنَّ وَطَرًا ۚ وَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ مَفْعُولًا ﴿٣٧﴾ مَّا كَانَ عَلَى النَّبِيِّ مِنْ حَرَجٍ فِيمَا فَرَضَ اللَّـهُ لَهُ ۖ سُنَّةَ اللَّـهِ فِي الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلُ ۚ وَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ قَدَرًا مَّقْدُورًا ﴿٣٨﴾ الَّذِينَ يُبَلِّغُونَ رِسَالَاتِ اللَّـهِ وَيَخْشَوْنَهُ وَلَا يَخْشَوْنَ أَحَدًا إِلَّا اللَّـهَ ۗ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ حَسِيبًا ﴿٣٩﴾ مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٤٠﴾

 

Na pale ulipomwambia yule ambaye Allaah Amemneemesha nawe ukamneemesha: Mshikilie mkeo, na mche Allaah! Na ukaficha katika nafsi yako ambayo Allaah Ametaka kuyafichua, na unakhofu watu, na hali Allaah Ana haki zaidi umkhofu. Basi Zayd alipomaliza haja kwake Tukakuozesha ili isiwe dhambi juu ya Waumini kuhusu (kuoa) wake wa watoto wao wa kupanga wanapomaliza haja kwao. Na Amri ya Allaah daima ni yenye kutekelezwa. Hakuna lawama yoyote juu ya Nabiy (kufanya) katika yale Aliyomfaridhishia Allaah, ni desturi ya Allaah kwa wale waliopita kabla. Na amri ya Allaah daima ni kudura iliyokwishakadiriwa vyema kabisa.  Wale wanaobalighisha ujumbe wa Allaah na wanamkhofu Yeye na wala hawamkhofu yeyote isipokuwa Allaah. Na Allaah Anatosheleza kuwa Mwenye kuhesabu. Hakuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Rasuli wa Allaah na ni mwisho wa Manabii. Na Allaah daima ni Mjuzi wa kila kitu. [Al-Ahzaab (33: 37, 40)]

 

Sababun-Nuzuwl:

 

 حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ الرَّحِيمِ، حَدَّثَنَا مُعَلَّى بْنُ مَنْصُورٍ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ زَيْدٍ، حَدَّثَنَا ثَابِتٌ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ ـ رضى الله عنه أَنَّ هَذِهِ، الآيَةَ ‏وَتُخْفِي فِي نَفْسِكَ مَا اللَّهُ مُبْدِيهِ‏ نَزَلَتْ فِي شَأْنِ زَيْنَبَ ابْنَةِ جَحْشٍ وَزَيْدِ بْنِ حَارِثَةَ‏.‏

 

Ametuhadithia Muhammad bin ‘Abdir-Rahiym, ametuhadithia Mu‘allaa bin Mansuwr toka kwa Hammaad bin Zayd, ametuhadithia Thaabit toka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه)  kwamba Aayah hii:

 

وَتُخْفِي فِي نَفْسِكَ مَا اللَّـهُ مُبْدِيهِ

Na ukaficha katika nafsi yako ambayo Allaah Ametaka kuyafichua.

 

Iliteremka kuzungumzia suala la Zaynab bint Jahsh pamoja na Zayd bin Haaritha”.

 

[Al-Bukhaariy katika Mujallad wa Kumi ukurasa wa 124]

 

[Al-Bukhaariy ameiandika tena Hadiyth hii katika Mujallad wa Kumi na Saba ukurasa wa 184 kutokana na Hadiyth ya Thaabit.  At-Tirmidhiy ameikhariji katika Mujallad wa Nne ukurasa wa 168 na kusema ni Swahiyh. Pia Ahmad katika Mujallad wa Tatu ukurasa wa 150, na Al-Haakim katika Mujallad wa Pili ukurasa wa 417. Adh-Dhahabiy ameiashiria kwa alama ya ufupisho wa Al-Bukhaariy na Muslim, kwa maana kuwa Hadiyth iko juu ya sharti lao wawili].

Na Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

فَلَمَّا قَضَىٰ زَيْدٌ مِّنْهَا وَطَرًا زَوَّجْنَاكَهَا

 

Basi Zayd alipomaliza haja kwake Tukakuozesha. [Al-Ahzaab (33:37)]

 

Na pia,

 

 أَخْبَرَنَا عَارِمُ بْنُ الْفَضْلِ. أَخْبَرَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ عَنْ ثَابِتٍ عَنْ أَنَسٍ قَالَ: نَزَلَتْ فِي زَيْنَبَ بِنْتِ جَحْشٍ:  ((فَلَمَّا قَضى زَيْدٌ مِنْها وَطَراً زَوَّجْناكَها))  قَالَ: فَكَانَتْ تَفْخَرُ عَلَى نِسَاءِ النَّبِيِّ  صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَقُولُ: زَوَّجَكُنَّ أَهْلُكُنَّ وَزَوَّجَنِي اللَّهُ مِنْ فَوْقِ سَبْعِ سَمَوَاتٍ.
 

Ametueleza ‘Aarim bin Al-Fadhwl, ametuhadithia Hammaad bin Zayd toka kwa Thaabit toka kwa Anas amesema: (Aayah hii) iliteremka kumhusu Zaynab bint Jahsh:

فَلَمَّا قَضَىٰ زَيْدٌ مِّنْهَا وَطَرًا زَوَّجْنَاكَهَا

Basi Zayd alipomaliza haja kwake Tukakuozesha

 

Akawa Zaynab anajifaharisha kwa wake wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwaambia: Watu wenu wamekuozesheni (kwa Rasuli), lakini mimi Allaah Ameniozesha (kwa Amri Yake) toka juu ya mbingu saba. [Ibn Sa‘ad katika Mujallad wa 8 sehemu ya Kwanza ukurasa wa 73 - Wapokezi wake ni wapokezi wa Swahiyh].

 

 

Na pia,

 

أَخْبَرَنَا عَفَّانُ بْنُ مُسْلِمٍ وَعَمْرُو بْنُ عَاصِمٍ الْكِلابِيُّ قَالا: حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ الْمُغِيرَةِ عَنْ ثَابِتٍ عَنْ أَنَسٍ بْنِ مَالِكٍ قَالَ: لَمَّا انْقَضَتْ عِدَّةُ زَيْنَبَ بِنْتِ جَحْشٍ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ  صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ  لِزَيْدِ بْنِ حَارِثَةَ: مَا أَجِدُ أَحَدًا آمَنَ عِنْدِي أَوْ أَوْثَقَ فِي نَفْسِي مِنْكَ. ائْتِ إِلَى زَيْنَبَ فَاخْطُبْهَا عَلَيَّ. قَالَ: فَانْطَلَقَ زَيْدٌ فَأَتَاهَا وَهِيَ تُخَمِّرُ عَجِينَهَا. فَلَمَّا رَأَيْتُهَا عَظُمَتْ فِي صَدْرِي فَلَمْ أَسْتَطِعْ أَنْ أَنْظُرَ إِلَيْهَا حِينَ عَرَفْتُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ قَدْ ذَكَرَهَا. فَوَلَّيْتُهَا ظَهْرِي وَنَكَصْتُ عَلَى عَقِبِي وَقُلْتُ: يَا زَيْنَبُ أَبْشِرِي. إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ يَذْكُرُكِ. قَالَتْ: مَا أَنَا بِصَانِعَةٍ شَيْئًا حَتَّى أُؤَامِرَ رَبِّي. فَقَامَتْ إِلَى مَسْجِدِهَا. وَنَزَلَ الْقُرْآنُ: ((فَلَمَّا قَضى زَيْدٌ مِنْها وَطَراً زَوَّجْناكَها))  

 

Ametueleza ‘Affaan bin Muslim na ‘Amri bin ‘Aaswim Al-Kilaabiy wamesema: Ametuhadithia Sulaymaan bin  Al-Mughiyrah toka kwa Thaabit toka kwa Anas bin Maalik amesema: Eda ya Zaynab bint Jahsh ilipomalizika, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  alimwambia Zayd bin Haaritha: “Sioni yeyote ninayemhisi sina wasiwasi naye kabisa kwangu na ninayemwamini zaidi katika nafsi yangu kuliko wewe. Nenda kwa Zaynab ukaniposee.” Zayd akaondoka haraka na akamkuta Zaynab anachanganya hamira unga wake.  (Zayd Anasema): Nilipomwona, nilihisi utukuzo na haiba kubwa kwake ndani ya kifua changu, sikuweza kumwangalia kwa kujua kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amemposa (na nikamwona kama ashakuwa mkewe, Mama wa Waumini). Nikageuka nisimwangalie na nikarudi nyuma kidogo na kumwambia: Ee Zaynab! Nimekuletea habari ya furaha. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) anakuposa. Akasema: Siwezi kumjibu kitu mpaka nimtake shauri Rabb wangu (niswali Istikhaarah). Akasimama na kwenda sehemu yake ya kuswalia, na hapo ikateremka Qur-aan:

 

 

فَلَمَّا قَضَىٰ زَيْدٌ مِّنْهَا وَطَرًا زَوَّجْنَاكَهَا

Basi Zayd alipomaliza haja kwake Tukakuozesha.

 

[Wapokezi wa Hadiyth hii ni wapokezi wa Swahiyh. Ahmad ameikhariji katika Mujallad wa 3 ukurasa wa 195, na Muslim ameikhariji katika Mujallad wa 9 ukurasa wa 228]

 

 

Share