016-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Nafasi Ya Shahaadah Mbili Katika Dini?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
016-Ni Ipi Nafasi Ya Shahaadah Mbili Katika Dini?
Swali:
س: ما محل الشهادتين من الدين
Ni ipi nafasi ya shahaadah mbili katika Dini?
Jibu:
ج: لا يدخل العبد في الدين إلا بهما
قال الله تعالى ( إنما المؤمنون الذين آمنوا بالله ورسوله )
وقال النبي صلى الله عليه وسلم ( أمرت أن أقاتل الناس حتى يشهدوا أن لا إله إلا الله وأن محمدا عبده ورسوله ) الحديث وغير ذلك كثير.
Mtu haingii katika Dini isipokuwa kwa Shahaadah hizo mbili. Allaah Anasema:
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ
Hakika Waumini ni wale waliomwamini Allaah na Rasuli Wake [An-Nuwr (24: 62)]
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema:
((أُمِرْتُ أن أقاتِل الناسَ حتى يَشهدُوا أن لا إله إلا الله ، أنَّ محمداً رسولُ الله...)
((Nimeamrishwa kupigana na watu mpaka washuhudie kuwa hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah na kwamba Muhammad ni Rasuli Wake)) [Al-Bukhariy na Muslim Hadiyth ya ‘Abdullaahi bin ‘Umar (رضي الله عنهما)]
Na Hadiyth nyenginezo zaidi ya hiyo.