017-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ipi Dalili Ya Kushuhudia Kuwa Hakuna Mwabudiwa Wa Haki Ila Allaah?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
017-Ipi Dalili Ya Kushuhudia Kuwa Hakuna Mwabudiwa Wa Haki Ila Allaah?
Swali:
س: ما دليل شهادة أن لا إله إلا الله
Ipi Dalili Ya Kushuhudia Kuwa Hakuna Mwabudiwa Wa Haki Ila Allaah?
Jibu:
ج: قول الله تعالى (شهد الله أنه لا إله إلا هو والملائكة وأولو العلم قائما بالقسط لا إله إلا هو العزيز الحكيم)
وقوله تعالى (فاعلم أنه لا إله إلا الله)
وقوله تعالى (وما من إله إلا الله)
وقوله تعالى (ما اتخذ الله من ولد وما كان معه من إله) الآيات
وقوله تعالى (قل لو كان معه آلهة كما يقولون إذا لابتغوا إلى ذي العرش سبيلا)
الآيات وغيرها.
Ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾
Allaah Ameshuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye; na (pia) Malaika na wenye elimu (kwamba Allaah) ni Mwenye kusimamisha (uumbaji Wake) kwa uadilifu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Aal-‘Imraan (3:18)]
Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ
Basi jua kwamba: laa ilaaha illa-Allaah (hapana muabudiwa wa haki ila Allaah) [Muhammad (47:19)]
Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿٦٥﴾
Na hakuna Muabudiwa wa haki yeyote isipokuwa Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika. [Swaad (38:65)]
Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
مَا اتَّخَذَ اللَّـهُ مِن وَلَدٍ وَمَا كَانَ مَعَهُ مِنْ إِلَـٰهٍ ۚ
Allaah Hakujifanyia mwana yeyote, na wala hakukuwa pamoja Naye mwabudiwa yeyote. [Al-Muuwminuwn (23:91)]
Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
قُل لَّوْ كَانَ مَعَهُ آلِهَةٌ كَمَا يَقُولُونَ إِذًا لَّابْتَغَوْا إِلَىٰ ذِي الْعَرْشِ سَبِيلًا ﴿٤٢﴾
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Kama ingelikuwa pamoja Naye waabudiwa kama wasemavyo; basi hapo wangelitafuta njia ya kumfikia Mwenye ‘Arshi. [Al-Israa (17:42)]
Na Aayah nyenginezo.