018-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah:Ni Nini Maana Ya Shahaadah Ya Laa Ilaaha Illa-Allaah
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
018-Ni Nini Maana Ya Shahaadah Ya Laa Ilaaha Illa-Allaah
Swali:
س: ما معنى شهادة أن لا إله إلا الله
Ni Nini Maana Ya Shahaadah Ya Laa Ilaaha Illa-Allaah?
Jibu:
ج: معناها: نفي استحقاق العبادة عن كل ما سوى الله وإثباتها لله عز وجل وحده لا شريك له في عبادته كما أنه ليس له شريك في ملكه
قال الله تعالى (ذلك بأن الله هو الحق وأن ما يدعون من دونه هو الباطل وأن الله هو العلي الكبير)
Maana yake ni: kukanusha kustahiki ‘ibaadah kwa kila kisichokuwa Allaah (سبحانه وتعالى) na kuithibitisha kwa Allaah (عز وجل) ni Mmoja Pekee Hana mshirika katika kuabudiwa Kwake, kama ambavyo Allaah (سبحانه وتعالى) Hana mshirika katika ufalme Wake.
Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ هُوَ الْبَاطِلُ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ ﴿٦٢﴾
Hivyo ni kwa kuwa Allaah Ndiye wa Haki, na kwamba vile wanavyoomba badala Yake ndiyo batili, na kwamba Allaah Ndiye Mwenye ‘Uluwa Uliotukuka, Mkubwa Kabisa. [Al-Hajj (22:62)]