Fataawaa Kuhusu Tahniyk (Kumrambisha Mtoto Mchanga Kitamu Kitamu)
Fataawaa Kuhusu Tahniyk (Kumrambisha Mtoto Mchanga Kitamu Kitamu)
Imaam An-Nawawiy, Imaam Ibn Baaz,
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahumu Allaah)
SWALI:
Ni wakati gani inafaa Tahniyk (Kumrambisha kitu kitamu mtoto mchanga?)
Imaam An-Nawawiy (Rahimahu Allaah): amesema:
“Tahniyk ni siku aliyozaliwa, ni Sunnah kwa makubaliano ya ‘Ulamaa.”
[Sharh Swahiyh Muslim lin-Nawawiy 14/123]
Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema: “(Tahniyk) Ni bora zaidi kufanywa siku ya kuzaliwa.’’
[Duruws Sharh Buluwgh Al-Maraam Kitaab Atw-Twa’aam].
Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
“Tahniyk inakuwa ni pale anapozaliwa tu, ili iwe cha mwanzo anachokula mtoto ni kile kitam alichorambishwa.’’
[Fataawaa Nuwr ‘Ala Ad-Darb Kanda (339)]