62-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ametumwa Kuondosha Yaliyokuwa Na Mashaka Na Magumu Kwa Watu

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

62-Ametumwa Kuondosha Yaliyokuwa Na Mashaka Na Magumu Kwa Watu

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٥٧﴾

Wale wanomfuata Rasuli; Nabiy asiyejua kusoma wala kuandika ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl, anawaamrisha mema na anawakataza munkari, na anawahalalishia vizuri na anawaharamishia maovu, na anawaondoshea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao. Basi wale waliomwamini na wakamtukuza, na wakamnusuru na wakafuata nuru (Qur-aan) ambayo imeteremshwa pamoja naye; hao ndio wenye kufaulu.  [Al-A’raaf: 157]

 

Imaam Ibn Kathiyr ameeleza katika Tafsiyr yake:

Kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ  

Na anawaondoshea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao.

 

Maana yake: Yeye Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) amewasahilishia watu kwa kuwandoshea yaliyo na taklifu.  Na minyororo iliyokuwa juu yao ni kwamba Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) amekuja kwa upole, ulaini na Dini nyepesi kama ilivyotajwa katika Hadiyth kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

أُرْسِلْتُ بِحَنِيفِيَّةٍ سَمْحَةٍ

 

Nimetumwa kwa Dini Ya Haniyfah (kuelemea haki tu) na (Dini) ya sahali ya uvumilivu.  [Musnad Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Asw-Swahiyhah)

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipowatuma Yemen amiri wawili Mu’aadh bin Jabal na Abu Muwsaa Al-Ash’ariyy  (رضي الله عنهما) aliwausia:

يَسِّرَا وَلَا تُعَسِّرَا وَبَشِّرَا وَلَا تُنَفِّرَا وَتَطَاوَعَا وَلَا تَخْتَلِفَا

 

Rahisisheni mambo kwa watu (kuhusu mambo ya Dini) wala msifanye magumu na toeni habari njema na msiwakimbize, na mtiiane (msikizane) wala msikhitilafiane.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Abu Barzah Al-Aslamiy Swahaba wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Niliambatana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nikaona jinsi gani alivyokuwa na usahali wa mambo. Ummah zilokuwa kabla yetu walifanyiwa mambo mazito katika Shariy’ah zao lakini Allaah Amefanya Shariy’ay ya jumuisho na sahali kwa Ummah huu, kama ilivyo kauli ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

إِنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ لأُمَّتِي عَمَّا وَسْوَسَتْ أَوْ حَدَّثَتْ بِهِ أَنْفُسَهَا، مَا لَمْ تَعْمَلْ بِهِ أَوْ تَكَلَّمْ ‏

“Hakika Allaah Amesamehe Ummah wangu (zile amali mbaya) ambazo nafsi zao huwanong’oneza au kupendekeza maadamu hawatatenda au kuzungumza.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Na pia amesema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

 رُفِع عَنْ أُمَّتِي اَلْخَطَأَ، وَالنِّسْيَانَ، وَمَا اسْتُكْرِهُوا عَلَيْهِ  رَوَاهُ اِبْنُ مَاجَهْ   

Umma wangu umeondoshewa kukosea, kusahau na walilolazimishwa.”  [Imetolewa na Ibn Maajah]  

 

 

Share